Thursday, October 18, 2012

WATUHUMIWA WA VURUGU MBAGALA WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Pichani juu ni namna watuhumiwa hao walivyofikishwa mahakamani

Watu 37 wakiwemo wanawake wawili wanaotuhumiwa kufanya vurugu kwa kuchoma makanisa, uharibifu wa mali na wizi wa kutumia nguvu jijini Dar Es Salaam ijumaa ya wiki iliyopita wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu mkazi kisutu  wakiwa chini ya ulinzi mkali.
Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani hapo wakiwa kwenye magari matatu ya polisi aina ya Defender jana saa 6 mchana wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevalia mabomu kiunoni, kutokana na kufanya matukio hayo kama sehemu ya kulipa kisasi kwa madai ya kunajisiwa kwa mkojo kwa kitabu cha Qur'an tukufu kulikofanywa na kijana wa kikristo.
Watuhumiwa hao wamefunguliwa kesi nne tofauti za jinai kwa mpigo, kesi ya kwanza ni jinai namba 240/2012, ya pili ni namba 241/2012, tatu 242/2012. nne 243/2012.
Watuhumiwa hao walisomewa mashitaka na mahakimu wakazi wawili ambao ni Sundi Fimbo anayesikiliza kesi tatu huku moja ikisikilizwa na Hakimu Bingi Mashabara.
Upande wa Jamhuri kwenye kesi hiyo uliwakilishwa na wakili mwandamizi Tumaini Kweka, Lasdlaus Komanya na Joseph Maugo.
Wakili Kweka alidai kuwa Oktoba 12 mwaka huu huko Mbagala watuhumiwa hao waliiba vitu mbalimbali ikiwemo Laptop, Printer Projector, Spika, Saa za ukutani na viti vya Plastiki mali ya kanisa la kiinjili la Kilutheri usharika wa Mbagala  vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Tshs Milioni 20
Aidha imeelezwa kuwa kabla ya kuiba watuhumiwa hao walimtishia mlinzi Michael Samwel kwa mashoka na nondo kwa lengo la kujipatia vitu hivyo.
Wakati huo huo mtoto aliyesababisha vurugu hizo amefikishwa katika mahakama ya watoto mbele ya Hakimu Devotha Kisoka akikabiliwa na shitaka moja la kuidhalilisha dini ya kiislam kwa kukikojolea kitabu cha Qur'an tukufu Oktoba 10.

No comments:

Post a Comment