Tuesday, October 9, 2012

ASIYEAMINIKA HAOLEWI AFUNGUKA NARGIS MOHAMED

Katika hali ya kuudhihirishia umma kuwa anaaminika ndiyo sababu iliyofanya mumewe achukue maamuzi ya kufunga naye pingu za maisha, Miss Tanzania No.3 2003/2004 Nargis Mohamed amefunguka kuwa mwanamke asiyeaminika hawezi kuolewa na kuongeza kuwa kwa upande wake anaamini kuwa ni mmoja kati ya wanawake wanaoaminika kwa sababu tayari ni mke wa mtu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Hotmix kinachoruka kupitia Eatv, Nargis ambaye hivi sasa amejikita kwenye Tasnia ya Filamu amesema ambavyo anafahamu yeye ni kwamba mwanamke anayeolewa ni yule anayeaminika na mwanaume anayemuoa na wala asiyefuata maneno ya kusikia pembeni na hata akisikia basi huuliza na kuyafanyia kazi maneno hayo.

Aidha Mrembo huyo alizungumzia kuhusu tabia ya wasichana wengi wa Bongo Movie kuandikwa kwa mambo mabaya mara kwa mara na kusema inawezekana kuwa tabia hizo zinatokana na wengi wao kutokwenda shule kwa sababu shule inasaidia pia kuyatafakari matendo unayofikiria kuyafanya.
 

No comments:

Post a Comment