Monday, October 29, 2012

MAPACHA WATATU WAKAMILISHA ALBUM YA PILI WAUKACHA WIMBO WA KALALA JUNIOR



Bendi ya Mapacha Watatu imekamilisha nyimbo za albamu ya pili ikiwa imeachana na wimbo wa Kalala Junior wa 'Mtoto wa Paka' uliotunga kabla ya kuikimbia.

Akizungumza jijini DSM, Khalid Chokoraa ambaye ni mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo alisema kuwa wameachana na wimbo wa Kalala kwa vile utaratibu wao hauruhusu kutumia wimbo uliotungwa na mwanamuziki aliyewakimbia.

"Ana uhuru wa kutumia wimbo wake huko aliko kwani ndivyo utaratibu wetu ulivyo, hatuwezi kurekodi wimbo wa mwanamuziki ambaye amechana nasi," alisema na kuendelea:

"Zipo nyimbo zetu ambazo tumekamilisha kwa ajili ya albamu ya pili ambazo ni ‘Wosia wa Babu’, ‘Naonewa’, ‘Chanzo Wanaume’, ‘Yarabi Nafsi’, ‘Mjasiriamali’, ‘Mjasiriamali', 'Sumu ya Mapenzi remix', 'Wivu' na  'Wosia wa Babu'.

Alisema kuwa kilichobaki sasa ni mipango ya kushuti video za baadhi ya nyimbo hizo ili zianze kurushwa kwenye vituo mbalimbali vya runinga kama sehemu ya utambulisho wa ujio wa albamu hiyo.

Aidha, Chokoraa alisema bendi hiyo haina ubaya wowote na Kalala Junior na kwamba wanaendelea kuheshimiana kama kawaida licha ya kwamba amewaacha na kurudi Twanga Pepeta.





No comments:

Post a Comment