Monday, October 29, 2012

Norman, Menynah Out Epiq BSS

Norman Severino
Zikiwa zimesalia  wiki mbili kufikia fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search, mchuano umezidi kuwa mkali baada ya wiki hii washiriki wawili, Norman Severino na Menynah Atik kuaga mashindano.

Washiriki hao wameaga na kuwaacha watazamaji midomo wazi, hali inayoonyesha shindano hilo limefikia patamu, kwani kila mshiriki aliyebaki ni mkali.

Kutoka kwa washiriki hao kuliwashtua hata majaji wenyewe, ambapo jaji Master Jay aliwatupia lawama Watanzania kwa kushindwa kuwapigia kura washiriki wenye vipaji.

“Hivi Watanzania mnajua kushindwa kupiga kura kwenu kuokoa washiriki wenye vipaji ndiko kulikofanya tumpoteze mshiriki mwenye kipaji kama Norman?" alisema Master Jay wakati akitangaza Norman ndiye anayeaga mashindano hayo.

Wanachi waliofika kushuhudia shindano la Jumapili katika studio za EBSS zilizoko Budget Hotel Kunduchi, nao walionekana kuzizima ghafla huku baadhi ya washiriki nao wakionekana kutokwa machozi, na kuzidi kutishika kwa hali ile.
Menynah Atik

Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwapa changamoto watazamaji kuwa kusikitika tu hakutasaidia washiriki wanaowapenda kubaki kwenye nyumba bali ni kura.

“Leo majonzi yametawala lakini ndo hivyo mimi nawasisitiza kila siku, ili mshiriki unayempenda asikutwe na hali hii… inabidi umpigie kura. Kura yako ndo kitu pekee kitakachomuokoa mshiriki ambaye wewe unaamini anastahili kuendelea kuwapo kwenye mashindano haya na mwishowe aje kuibuka mshindi wa shindano hili,” alisisitiza Ritha.

Washiriki wengine walioingia katika Danger Zone wiki hii ni Godfrey Kato mwenye namba za ushiriki EBSS 01, Husna Nassoro mwenye namba EBSS 02, Nshoma Ng’hangasamala mwenye namba EBSS 07 na Walter Chilambo (EBSS 12). 

Watanzania wameombwa kupiga kura kuwaokoa washiriki wanaowapenda kwa kuandika EBSS unaacha nafasi kisha unaandika namba ya mshiriki kwenda 15530.



 

No comments:

Post a Comment