Wednesday, October 10, 2012

MSONDO NGOMA KUANGUSHA BURUDANI MIKOA YA KUSINI

BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini Msondo ngoma Music Band kesho itafanya onyesho la nguvu katika Ukumbi wa Jumba la maendeleo ya Wananchi, Utete wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo Said Kibiriti, alisema onyesho hilo ni sehemu ya ziara yao katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.


Baada ya kuwapa burudani watu wa pwani watahamia katika Ukumbi wa Lindi beach resort uliopo mjini Lindi ambapo Jumamosi inatarajia kukonga nyoyo za mashabiki wake katika Ukumbi wa Makonde beach club mjini Mtwara.

Baada ya onyesho la mjini Mtwara, siku ya maadhimisho ya kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Oktoba 14, bendi hiyo itaelekeza itaangusha burudani katika Ukumbi wa Emirates uliopo wilayani Masasi
Bendi hiyo itahitimisha ziara yake siku ya Jumatatu Oktoba 15, mjini Nachingwea kwa kufanya onyesho katika ukumbi wa Nachingwea resort.

No comments:

Post a Comment