Tuesday, October 9, 2012

TMF YAWANOA WANAHABARI MKOANI LINDI

Pichani juu ni baadhi ya wanahabri mkoani Lindi wakifuatilia mafunzo
Katika kuimarisha na kukuza uimara wa vyombo vya habari nchini, Mfuko wa vyombo vya habari Tanzania(TMF) umetoa mafunzo kwa waandishi na wamiliki wa vyombo vya habari mkoani Lindi ili kuwajengea uwezo wa kuomba Ruzuku zinazotolewa na mfuko huo kufuatia awamu ya pili ya utoaji wa Ruzuku hizo. mafunzo hayo yaliyotolewa jana yaliendeshwa na mwandishi mkongwe na mshauri wa mambo ya habari Bw. Ndimara Tegambwage (pichani juu)na Meneje wa vyombo vya habari vya SJMC ambaye pia ni mwandishi mkongwe Bi. Edda Sanga... Source-www.lindiyetu.blogspot.com



No comments:

Post a Comment