Mrembo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye kinyang'anyiro cha Miss East Africa mwaka huu ni mwanadada JOCELYNE DIANA MARO (22).
Mlimbwende huyo alipatikana ndani ya mchakato ulioendeshwa na kamati maalum ya kuratibu zoezi hilo, kwa zaidi ya miezi mitatu iliyopita na kuwashinda warembo wengine 148 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss East Africa 2012
Maandalizi ya mashindano hayo yanaendelea vizuri na yapo kwenye hatua za mwisho ikiwa ni pamoja na kukamilisha taratibu zote za BASATA ili kufanikisha mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 07 December, 2012 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Nchi zilizothibitisha kushiriki mashindano hayo ni wenyeji Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine zilizoalikwa kushiriki ni pamoja na Ethiopia, Eritrea, Somalia, Djibouti, Southern Sudan, Malawi, pamoja na visiwa vya Seychelles, Madagascar, Reunion, Comoros, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanalenga kukuza ushirikiano na kutangaza utamaduni wa Afrika Mashariki, pamoja na kutangaza utalii wa Tanzania kama Nchi wenyeji wa mashindano hayo makubwa katika ukanda huu wa Afrika.
Mashindano ya Miss East Africa yanamilikiwa na kuandaliwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam,.
No comments:
Post a Comment