Tuesday, October 16, 2012

Wacheza uchiwa Filamu za kibongo waiangukia jamii

Wema Sepatu akiomba msamaha kwajamii mbele  ya Waandishi  wa Habari


Wasanii hao walisema kwamba wamelazimika kuvaa vijivazi hivyo, kulingana na wakati na hasa kwenye matukio husika huku wakijitetea kwamba tatizo lilikuwa ni urefu wa jukwaa.

Kwa upande wa Aunt Ezekiel alisema kwamba  kilichotokea ni bahati mbaya, kwani hawana uzoefu na majukwaa ya muziki na matokeo yake kuwa hivyo.

Mbali na Mastaa hao kuomba radhi kutokana na kitendo hicho cha kuvaa Uchi, ndani ya tamasha la Fiesta la mwaka huu 2012 wasanii hao wa Filamu nchini  Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamesema kwamba wataendelea kuvaa nguo hizo.
Aunt Ezekiel

Wakilonga nawaandishi wa habari ndani ya Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), hapa Jijini wasanii hao walikiri kufanya tukio hilo wasilolitarajia wkamba lingetokea siku hiyo.

Mmoja ya wasanii hao, Aunt Ezekiel alisikika akisema kwamba kilichotokea ni bahati mbaya kwani hawana uzoefu na majukwaa ya muziki na matokeo yake kuwa hivyo.

Alisema kwamba mavazi hao wanayavaa kila mara, lakini kwa bahati mbaya jukwaa lilikuwa refu na ndiyo maana walionekana wakiwa wamevaa utupu kwani wameomba msamaha kwa mashabiki wao na kwa jamii iwazungukayo kwa ujumla.

Huyo ni Aunt Ezekiel akiwa katka mavazi hayo yaliyokuwa gumzo kwa jamii

"Tunapenda kuchukua fursa hii kuiomba radhi jamii yote, ndugu jamaa na marafiki kwa tukio hili ambalo hatukulitarajia,” alisema Aunt Ezekiel.

Akizungumzia tabia yake ya kupiga picha za utupu, Aunt alikana na kudai kwamba; “Hizo picha wanazodai ni za utupu si kweli, bali nilipigwa mgongo kwa ajili ya jalada la filamu ya Young Millionea.

Hizo nguo fupi sijaanza kuvaa jana wala juzi, hivyo kwa tukio lile ilitokea bahati mbaya na kuanzia sasa nitakuwa makini na vitu kama hivyo,” alisema Aunt Ezekiel.

Naye Wema, pamoja nakuomba radhi aliitaka jamii kutowachukulia vibaya kutokana na mavazi hayo, kwani mara nyingi wanavaa kulingana na wakati na mahali.
Wema  Sepetu akiwa ndani ya vivazi hivyo

Alisema baada ya dosari hizo kujitokeza, aliamua kuanza kuvaa suruali za jeans au kaptula ili kuepukana na kitendo hicho.

Kwa upande wake Katibu wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Wilson Makubi alisema baada ya tukio la wasanii hao, waliwaita na kuzungumza nao na mwisho wa siku walikiri makosa na wakaomba radhi.
Wema Sepetu na Aunt Ezekiel 


No comments:

Post a Comment