Pichani juu baadhi ya matukio yaliyotokea zanzibar mchana wa leo
Siku chache baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni Waumini wa dini ya
kiislamu kufanya vurugu kufuatia mtoto mmoja kukojolea kitabu cha
Qur'an na kusababisha jeshi la polisi kuwakamata watuhumiwa zaidi ya
37 na kuwafikisha mahakamani, leo limeibuka jipya baada ya watu
wengine wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Sheikh Issa Ponda kuandamana
kuelekea katika kituo cha Polisi kati jijini Dar Es Salaam.
Watu hao wameandamana kupinga kukamatwa kwa katibu wa Jumuiya na
Taasisi ya kiislam Sheikh Issa Ponda ambaye alikamatwa jana usiku na
kushinikiza aachiwe huru, wamesababisha askari Polisi kutanda katika
eneo hilo na kulazimika kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya
watu hao ambao hata hivyo walionekana kukataa kuondoka katika eneo
hilo mpaka Katibu wao huyo aachiwe huru.
Sheikh Ponda amekamatwa kufuatia tuhuma mbalimbali zikiwemo za
kuhusika na uchochezi kwa serikali iliyopo madarakani na kuchochea
vurugu za udini baina ya waislam na wakristo likiwemo tukio lile la
Mbagala lililotoke hivi karibuni Mbagala jijini DSM.
Wakati huo huo wafuasi wa kundi la uamsho wamefanya vurugu kufuatia
kile kilichodaiwa kuwa ni kutekwa kwa kiongozi wao wa kundi la
uamsho, jambo lililowalazimu Polisi kutumia mambomu ya machozi
kuwasambaratisha wafuasi hao.
|
No comments:
Post a Comment