Wednesday, October 17, 2012

Kunani Rukky na Tonto?

                         
Rukky Sanda ameibuka na kumtetea msanii mwenzie mtata, Tonto baada ya mashabiki kumwambia aache muziki na kwamba hajui lolote.

Wasanii hao wawili ni maswahiba wa siku nyingi na hawana uhusiano mzuri na wasanii wengine. Mashabiki wamemvamia Tonto kwenye mtandao wa Twitter na kuponda nyimbo zake kwa madai kuwa hajui kitu wala hana kipaji.

"Tonto Dike ni mwimbaji mzuri, kwanini msiwe na subira mkamsikiliza kwanza kabla ya kumkosoa?," alisema Rukky ambaye ameahidi kutoa filamu tatu mpya kabla mwaka haujaisha.

No comments:

Post a Comment