Friday, October 12, 2012

SIWEZI KUFANYA KAZI NA NIKKI MBISHI AFUNGUKA NIKKI WA PILI

Nikki wa pili katika pozi

Mmoja kati ya wasanii wanaounda kundi la muziki la weusi ambae pia ni mdogo wa mwana Hip Hop nguli nchini, Joh Makini, amefunguka kuwa yupo tayari kufanya kazi na mwanamuziki yeyote lakini si mwana Hip Hop mwenzake Nikki mbishi.

Akizungumza jana ndani ya kipindi cha Hotmix cha Eatv Nikki alisema ameamua hivyo kutokana na kugundua kuwa mwanaHip Hop huyo hathamini kile yeye(Nikki wapili) anachokifanya.

"Naweza kufanya kazi na mwanamuziki yeyote hapa Bongo lakini siwezi kufanya kazi na Nikki mbishi hata tukipatana, kwa sababu yeye hathamini kazi yangu ninayoifanya" sasa kama mtu hathamini unachokifanya kwa nini ufanye naye kazi? alihoji Nikki wa kwanza.

Nikki alizungumza hayo kutokana na swali aliloulizwa kwenye kipindi hicho kuwa kutokana na bifu linaloendelea kati yao ikitokea Nikki mbishi akaamua mambo yaishe na wafanye kazi pamoja ataamua nini(atakubali au atakataa
)

No comments:

Post a Comment