Monday, October 22, 2012

Aisha Madinda asaka kibarua




Aisha Mbegu 'Madinda' akiwa kikazi zaidi  hapo ni kabla hajaokoka

 Kwa sasa mnenguaji huyo anasali ndani ya Kanisa la Kilokole la Zoe lililopo maeneo ya Tabata hapa Jijini, kwani alisema kwamba ameanza kusaka kibara kwenye maofisi mbalimbali kupitia vyeti vyake.


Hiyo ni baada ya kuamua kuokoka, mnenguaji aliyejizolea umaarufu  kwenye muziki wa dansi Aisha Mbegu 'Madinda', alisema kwamba kwa sasa anasaka kibarua kingine cha kufanya huku akimtumikia Mungu.

Kwani aliweza kujisalimisha kwenye  kanisani mara tu baada ya kusumbuliwa na miguu kwa muda mrefu, na kufanikiwa kupona ndipo akaona ni bora aachane na kazi ya muziki wa kidunia ili atafute kibarua kingine cha kufanya.

"Tangu niombewe nimepona kabisa na sasa miguu imetulia na nimeona niachane na muziki ili nitafute kazi nyingine ambayo haiwezi kuniingiza kwenye matatizo," alisema mnenguaji huyo.

Mbali na hilo anamshukuru mtu aliyempa ushauri wa kwenda kwenye kanisa hilo, ambalo amedai kuwa limemsaidia kupona maradhi yake ya miguu na kwamba anaendelea kwenda katika kanisa hilo kila Jumapili.

"Kwa zaidi ya miaka miwili nimekuwa nikisumbuliwa na miguu kila ninapopanda jukwaani kucheza, lakini baada ya kwenda kuomba nimekuwa fiti ndio maana nikaamua kuacha muziki ili nifanye kazi nyingine," alisema.


No comments:

Post a Comment