Friday, October 5, 2012

LIVA HASSAN NA ALLAN MULUMBA KUUNGANA USIKU WA SAUTI NA MARAFIKI WA KWELI

Allan Mulumba kushoto na Liva Hassan
Baada ya kutokutana kwa takribani miaka kumi na tatu, wanamuziki waliofanya kazi kwa pamoja enzi hizo wakiwa na Bendi ya Diamond Sound, wanamuziki mahiri Liva Hassan Mfalme na Allain Mulumba Kashama wanatarajia kuvaana kwenye Steji moja Siku ya usiku wa sauti na marafiki wa kweli utakaofanyika katika ukumbi wa Princess.

Kiongozi wa kundi hilo Ibonga Katumbi amesema tayari wameshafanya mazungumzo na Liva Hassan na amekubali kuungana nao katika siku hiyo maalum ambayo itawakutanisha wasanii hao baada ya kutengana kwa miaka 13 sasa.

Aidha Ibonga amewataka mashabiki kusubiri kwa hamu siku hiyo kwani wanamuziki hao watafanya mambo makubwa katika kutoa burudani kwa mashabiki na wapenzi wao.

No comments:

Post a Comment