Monday, October 15, 2012

TOP MODEL YAENDA KWA MAGDALENA ROY

.
Top Model akipita jukwaani


 Miss Dar City Centre ambaye pia alishika nafasi ya pili katika shindano la Redd’s Miss Ilala, Magdalena Roy amekuwa mrembo wa pili kuingia katika 15-Bora ya mashindano ya Redd’s Miss Tanzania 2012 baada ya kutwaa taji dogo la Top Model juzi usiku.

Magdalena anaungana katika hatua hiyo na Miss Mbulu, Lucy Stephano, ambaye wiki iliyopita alitwaa taji la Miss Photogenic.

Shindano la Top Model lililofanyika kwenye hoteli ya Naura Spring jijini Arusha lilikuwa na upinzani mkali likishirikisha warembo wote 30 wa Redd’s Miss Tanzania 2012.

Mbali na Magdalena, warembo wengine walioifikia hatua ya tano bora ya Top Model walikuwa ni Mary Chizi (Ilala), Irene Veda (Lindi), Belinda Mbogo (Dodoma) na Sina Revocatus (Elimu ya Juu).

Akizungumza na jijini humo , Afisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania, Haidan Ricco alisema warembo hao jana waliondoka kuelekea Tanga kwa ajili ya kutembelea mapango ya Amboni, kabla ya kurejea Dar es Salaam.

Magdalena Roy anayepunga mkono akiwa na washindi wenzake baada ya kutangakwa kuwa ndiye Top Model

Warembo 30 wanawania taji la Redd’s Miss Tanzania, ambalo kwa sasa linadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd’s Original.



No comments:

Post a Comment