Wednesday, October 17, 2012

WAJUE MASTAA WANAOISHI MAISHA YA VITUKO


   
     
 


Kuna wasanii 12 wa kike wa Nollywood waliokumbwa na kashfa hivi karibuni. Kashfa hizo zinatokana na kuhusishwa kwao na mambo mbalimbali huku vituko vyao vikiibua maswali mengi kwa jamii.

Mercy Johnson
Mercy Johnson alivuma hata kabla ya kuolewa na Prince Odi Okojie mwezi Agosti mwaka jana. Picha zake za uchi zilizagaa kwenye mitandao kadhaa na magazeti ya udaku.

Harusi yake ndio ikavuma zaidi kwa madai kuwa alimpiku mwanamke mwingine ambaye alikuwa aolewe na Prince.

Ini Edo
Hata yeye ameandamwa na kashfa za ngono, awali kabla hajaolewa, ilivumishwa kwamba alikuwa mchumba wa bosi mmoja wa majimbo ya kusini mwa Nigeria.

Ingawa ameolewa lakini hivi karibuni ameonekana klabu ya usiku na mwanaume mwingine.

Tonto Dikeh
Kila mara yupo kwenye magazeti tangu mwaka 2006 alipoanza kuvuma. Leo utamsikia na kashfa ya ulevi, kesho kagombana na mtu. Kwenye mwili wake amechora tattoo 57 za aina mbalimbali.

Ni mvutaji sigara mahiri na aliwahi hata kumkera Van Vicker wakati fulani kwa tabia hiyo.

Iyabo Ojo
Alikuwa na bifu na msanii mwenzake, Lizzy Anjorin mpaka wakafikia hatua ya kutishiana kulogana, lakini wakapatanishwa na kigogo mmoja wa serikali.

Habari zilizoripotiwa hivi karibuni ni kwamba alikutwa akifanya mambo ya ajabu na mwanaume mmoja kwenye gari jijini London na picha zikasambazwa.

Funke Akindele
Alivumishiwa mambo mengi sana, lakini kikubwa ni hivi karibuni iliporipotiwa kwamba ameolewa na kuwa mke wa tatu kwa mumewe. Lakini yeye hana matatizo na hilo.

Genevieve Nnaji
Genny, kama anavyopenda kuitwa, amehusishwa kuwa na uhusiano na wasanii kama Ramsey Nouah, RMD na Pat Attah.

Ni miongoni mwa wasanii wenye mambo mazito ya nyuma ya pazia ambayo hayawezi kusahaulika ikitajwa kwamba ni mlevi na mvutaji mahiri.

Tayo Odueke (Sikiratu Sindodo)
Ametuhumiwa kuwa na uhusiano na vigogo wengi wa Serikali mpaka wengine wakampeleka nje kuhiji. Ingawa amekuwa akikanusha, lakini vituko vyake vya mara kwa mara vimemfanya asipotee kwenye uso wa jamii.

Stella Damasus
Alikuwa anachukuliwa kama msanii mtulivu, lakini madai kwamba amevunja ndoa ya staa mwenzake, Doris Simeon, yamemchafua. 


Wawili hao wamekuwa wakikanusha, lakini ukaribu wao umeibua maswali mengi kama kweli ni biashara tu au kuna mengine?

Bukky Wright
Ni mama wa watoto wawili ambaye kuvunjika kwa ndoa yake kutokana na vituko vyake, kulimweka pabaya na akaanza kuonekana kama mtu wa ajabu. Hajaolewa tena mpaka sasa.

Faithia Balogun
Matukio yake ya kutwangana ngumi na wasanii wenzake ni mengi kuliko mazuri yaliyoripotiwa. Ameachana na mumewe, lakini bado anaendelea kutumia jina la ukoo wa mwanaume huyo na kulea watoto wake wawili.

Stephanie Okereke
Alichapana makonde na Genevieve Nnaji mwaka jana kwa madai kwamba alikuwa akimmendea mumewe. Inadaiwa kuwa hajiskii vizuri Genevieve kuwa karibu kiutendaji na kiharakati na Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan.

Mosun Filani
Alimng'oa mumewe kwenye uhusiano mwingine ambao ulikuwa na watoto wawili. Lakini wiki chache baada ya ndoa yake, mwanaume wake wa zamani akamuamuru amrudishie gari yake aliyokuwa amemnunulia na akairudisha kwa aibu.

Mume wa Omotola afukuzwa kazi

LAGOS, NIGERIA
MUME wa staa wa filamu za Nollywood, Omotola Jalade- Ekehinde, ambaye ni rubani wa Shirika la Ndege la Air Nigeria, amepigwa chini.

Wafanyakazi 800 wa shirika hilo wamepunguzwa kazi hivi karibuni kwa maelezo ya utendaji usioridhisha, kati ya waliokumbwa na balaa hilo ni baba huyo wa watoto wanne.

Rafiki wa karibu wa bwana huyo, amedai kuwa mume huyo wa Omotola ni mtu wa kujituma sana, lakini hivyo ni bahati mbaya kwake kufukuzwa kazi.

Katika hatua nyingine, Omotola ameajiri mawakili mahiri wa Nigeria ambao watamtetea kwenye kesi yake ya kukiuka masharti ya mkataba na kampuni moja ya filamu.

Kwa mujibu wa walalamikaji msanii huyo ameshindwa kuheshimu mkataba aliouingia mwaka 2010.

Genevieve abambwa akivuta sigara
LAGOS, NIGERIA 

 
Mmoja wa maprodyuza wa Nigeria, Charles Novia, amefichua siri kwamba mwanadada, Genevieve Nnaji, anavuta sigara na ni mtu wa kujipakaa poda.
Novia amefichua kwamba alimbamba msanii huyo kwenye kona moja ya jengo walilokuwa wakijiandaa kupiga picha za filamu yake mpya.

"Wakati mafundi wakiseti mitambo, nikatoka nje kidogo kupata hewa safi, ghafla nikamwona Genevieve anavuta sigara akashtuka akasema �Whoops! umenibamba," alisema Novia.

"Nikamuuliza unavuta? Akaniuliza nawe unavuta, nikamwambia sivuti, lakini sina matatizo na watu wanaovuta. Lakini nikamshauri ajitahidi kuacha kutokana na madhara ya kiafya.

"Akanijibu kwamba anajaribu kuacha, ndio akaniambia nikae karibu yake tujadiliane mambo ya filamu ambayo tulikuwa tunaiandaa lakini muda wote ni mtu wa kujipaka poda sana. Kifupi ni kwamba anaupenda sana uso wake."

Heh! Nitembee na kijana mimi?
LAGOS, NIGERIA

SHAN George amekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mvulana wa miaka 21 akisisitiza kuwa hayo ni majungu tu na ameomba aachwe na maisha yake.

Msanii huyo anadai kwamba kuna watu wanamwonea wivu kutokana na maendeleo yake ndio maana wanataka kuchafua heshima yake mbele ya jamii.

"Wamemaliza kumsingizia Mikel Obi sasa wamehamia kwangu. Lazima nipige hatua kwenye maisha na watu ndicho kinachowauma wanaanza kusingizia mambo ya ajabu,"alisisitiza.

"Watashindwa kwa vile mimi nazidi kufanikiwa kimaisha kwa msaada wa Mungu, Mungu awasamehe tu. Mimi sina uhusiano wowote na watoto wa Tee Mac." Mwanaume huyo naye alikana kuwa na uhusiano na Shan.

No comments:

Post a Comment