|
Norman Severino |
Zikiwa zimesalia wiki mbili kufikia
fainali za shindano la Epiq Bongo Star Search, mchuano umezidi kuwa
mkali baada ya wiki hii washiriki wawili, Norman Severino na Menynah
Atik kuaga mashindano.
Washiriki hao wameaga na kuwaacha watazamaji midomo wazi, hali
inayoonyesha shindano hilo limefikia patamu, kwani kila mshiriki
aliyebaki ni mkali.
Kutoka kwa washiriki hao kuliwashtua hata majaji wenyewe, ambapo jaji
Master Jay aliwatupia lawama Watanzania kwa kushindwa kuwapigia kura
washiriki wenye vipaji.
“Hivi Watanzania mnajua kushindwa kupiga kura kwenu kuokoa washiriki
wenye vipaji ndiko kulikofanya tumpoteze mshiriki mwenye kipaji kama
Norman?" alisema Master Jay wakati akitangaza Norman ndiye anayeaga
mashindano hayo.
Wanachi waliofika kushuhudia shindano la Jumapili katika studio za EBSS
zilizoko Budget Hotel Kunduchi, nao walionekana kuzizima ghafla huku
baadhi ya washiriki nao wakionekana kutokwa machozi, na kuzidi kutishika
kwa hali ile.
|
Menynah
Atik |
Jaji mkuu wa shindano hilo, Ritha Paulsen, aliwapa changamoto watazamaji
kuwa kusikitika tu hakutasaidia washiriki wanaowapenda kubaki kwenye
nyumba bali ni kura.
“Leo majonzi yametawala lakini ndo hivyo mimi nawasisitiza kila siku,
ili mshiriki unayempenda asikutwe na hali hii… inabidi umpigie kura.
Kura yako ndo kitu pekee kitakachomuokoa mshiriki ambaye wewe unaamini
anastahili kuendelea kuwapo kwenye mashindano haya na mwishowe aje
kuibuka mshindi wa shindano hili,” alisisitiza Ritha.
Washiriki wengine walioingia katika Danger Zone wiki hii ni Godfrey Kato
mwenye namba za ushiriki EBSS 01, Husna Nassoro mwenye namba EBSS 02,
Nshoma Ng’hangasamala mwenye namba EBSS 07 na Walter Chilambo (EBSS 12).
Watanzania wameombwa kupiga kura kuwaokoa washiriki wanaowapenda kwa
kuandika EBSS unaacha nafasi kisha unaandika namba ya mshiriki kwenda
15530.