Thursday, July 28, 2011

CHIDY BENZ AIKACHA BANGI

CHIDY BENZ
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya CHIDY BENZ, ambae pia ni Star wa kipindi cha Chidy Show kinachorushwa na EATV ameweka wazi kuwa ameachana na uvutaji wa bangi a.k.a kijiti au majani.

Akiongea na Blog hii leo asubuhi Chidy Benz amefunguka kuwa ameamua kuachana na kilevi hicho kwa kuwa hakina faida yoyote kwake zaidi ya hasara inayotokana na ukorofi wake kila anapotumia kilevi hicho.

Chidy aliendelea kuweka wazi kuwa alianza kutumia bangi tangu akiwa mdogo wakati akiwa shuleni ambapo alikuwa akivuta kwa wingi na mpaka leo hajawahi kuona faida yake na akaongeza kuwa mara nyingi amekuwa akichelewa kwenye vikao na wasanii wenzake lakini chanzo kikuu ni utumiaji wa Bangi, hivyo amegundua kuwa kilevi hicho kinamuharibia mipango yake mingi ndipo akaona ni busara kuachana nacho.

Hata hivyo ameahidi kuwa hivi karibuni atatangaza kuachana na ulevi wa Pombe, ingawa ameweka wazi kuwa bado hajafanya maamuzi kwa kuwa uamuzi huo anahisi kuwa ni mgumu japokuwa anaendelea kuufanyia kazi taratibu.

YOUSSOU N'DOUR NA ANGELIQUE KIDJO KUPIGA SHOW TUNISIA

YOUSSOU N'DOUR KUTOKASENEGAL
ANGELIQUE KIDJO KUTOKA BENIN
Wanamuziki maarufu Barani Africa YOUSSOU N'DOUR kutoka Senegal na ANGELIQUE KIDJO kutoka Benin wanatarajia kupiga Showa ya pamoja katika Concert moja huko nchini Tunisia.

Show hiyo kali ambayo itahusisha pia Wasanii wengine kutoka Tunisia imeandaliwa na Mo Ibrahim Foundation na inatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu ambapo itafanyika mbele ya viongozi wa dunia kwa ajili ya kutambua mchangio wa vijana wa Nchi hiyo kwa Nchi yao 

SOURCE:Chini ya carpetblogspot

Tuesday, July 26, 2011

MAJALIWA KUTIMKIA MLIMANI PARK

SHUKURU MAJALIWA

MAJALIWA katikati akiwa na ROMARIO wakati akiwa na bendi ya Msondo Ngoma

Aliyekuwa mwanamuziki wa Msondo Ngoma Music Band(Baba ya Muziki) SHUKURU MAJALIWA ameihama bendi yake hiyo na kutimkia DDC Mlimani Park(Wana sikinde ngoma ya ukae).


Habari zaidi za kwa nini ameamua kuihama msondo na kukimbilia Sikinde sijazipata bado ila naendelea kufuatilia kwa umakini zaidi ili niweze kukujuza, endelea kutembelea hapa ili upate undani zaidi, pia usikose kufuatilia kwenye afrobeat utamsikia pia mwenyewe akizungumza mara baada ya kumpata.

Monday, July 25, 2011

MR. NICE AWAPONDA WALIOSEMA KAFULIA ATAMBA KURUDI KWA KASI

Mr. NICE na mwimbaji wake AMINA CHONCHOLICHO wakiimba kwa pamoja

Mr. NICE akiimba akiwa katikati ya wanenguaji wake wa Bush band

Mr. NICE akikumbushia enzi zake mashabiki kwa kucheza
Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambae alikuja juu kwa Style yake ya TAKEU miaka kadhaa iliyopita Mr. NICE (Mfalme wa Takeu) ametamba kurudi tena kwa kasi huku akiaidi kuwafunga midomo wale wote waliokuwa wakisema kuwa amefulia na hana jipya tena, Nice na Band yake inayofahamka kama Bush Band hupiga Show kila jumapili katika Hotel ya DEN FRENCE iliyopo Sinza jijini DSM.


Picha kwa Hisani ya Global Publishers

Sunday, July 24, 2011

ONYESHO LA TWANGA KUMCHANGIA MAALIM GURUMO LAFANIKIWA

Maalim GURUMO akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa ASET ASHA BARAKA na Wana ASET kwa onyesho hilo maalum kwa ajili ya kumchangia ambalo limefanyika Jumamosi ya July 23 katika ukumbi wa Mango Garden DSM.

Mkurugenzi wa ASET, ASHA BARAKA akifuatilia maongezi ya NAIBU MEYA wa Manispaa ya kinondoni Mh. SONGORO MNYONGE wakati wa Onyesho hilo

ASHA BARAKA akikabidhi mchango uliochangwa na wadau kwa MAALIM GURUMO

Kiongozi wa Msongo Ngoma SAID MABERA akimpa Support mzee mwenzie

Mashabiki na Wadau wa muziki wakiwa na baadhi ya waimbaji wa msondo ngoma.

Friday, July 22, 2011

TOTOO ZE BINGWA KUZINDUA HII MAMBO HAIELEWEKI KESHO

Rapa aliyejipatia umaarufu mkubwa hapa nchini kupitia bendi yake ya Akudo Impact, TOTOO ZE BINGWA kesho anatarajia kuzindua album yake inayofahamika kwa jina la Hii Mambo haieleweki.  



Akizungumza na BLOG hii TOTOO ZE BINGWA amesema Album hiyo ina nyimbo nane ambazo ni dozi, sina neno lingine,Discipline,amekubalika,Jamani,Siku hiyo,World Cup na Hii mambo haieleweki iliyobeba jina la Album hiyo.

Mali na uzinduzi wa Album hiyo pia anatarajia kuzindua kikundi chake cha Sanaa kinachojulikana kwa jina la "sanaa sanaa" na Uzinduzi huo utasindikizwa na Bendi yake ya Akudo Impact, Benjamin wa Mambo Jambo, 20% na Wanamuziki wengine kutoka nchini Kenya.

MARY KHAMIS KUTIKISA KATIKA ONYESHO LA KUMCHANGIA GURUMO

Mshindi wa Shindano la manywele kimwana wa Twanga pepeta 2011 "MARY KHAMIS" kesho anatarajia kuungana na Bendi yake ya Twanga pepeta na Msondo Ngoma katika Onyesho la kumchangia Mwimbaji mkongwe MUHIDINI GURUMO ambae amekuwa akiugua kwa muda mrefu
Akizungumza na AFROBEAT ya EATV Mkurugenzi wa African Stars Entertainment(ASET) ASHA BARAKA, amesema lengo la onyesho hilo ambalo limeandaliwa na ASET kupitia Bendi yake ya Twanga pepeta ni kuchangisha pesa za kumsaidia Muimbaji huyo mwenye heshima kubwa hapa Nchini, kwa ajili ya Matibabu na Kujikimu katika matumizi yake ya kawaida.

Thursday, July 21, 2011

HAPPY BIRTHADAY AMALLU

Anaitwa HALIMA FRED a.k.a AMALLU ni Producer wa SKONGA Show ya Eatv, leo ni siku yake muhimu sana kwa kuwa siku kama ya leo miaka kadhaa iliyopita ndipo alizaliwa. Hivyo nachukua nafasi hii kumpongeza kwa kuongeza umri wake leo ila napenda kumwambia kuwa akumbuke kuwa umri unapoongezeka ndipo majukumu yanaongezeka so JIPANGE MAMA..... HAPI B'DAY MA' LUV

Wednesday, July 20, 2011

UNAIONAJE HIIIIIIIII???????

Jamani si vibaya ukipenda kitu ukasema, kwa upande wangu nimependa sana jinsi alivyovaa mwanadada huyu mpaka akanisukuma kushare na wewe kile ambacho mimi nimekiona kutoka kwake.... Kwa kweli amependeza mnooooooooo!!! roho mbaya haijengi jamani.... SALUTE kwako MWAMVITA MAKAMBA........ PICHA kwa hisani ya JIACHIE

TAMASHA LA 17 LA MZANZIBAR LAZINDULIWA LEO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mh. MOHAMED ABOUD akihutubia wakati wa ufunguzi wa Tamasha hilo la 17 la Mzanzibar, lililofanyika katika ufukwe wa pwani ya Nungwi
Mh. MOHAMED ABOUD akizindua rasmi Tamasha hilo kwa kupiga bastola juu
Waimbaji wa Taarabu wa kikundi kutoka Zanzibar wakitumbuiza katika Tamasha hilo

SENATOR JACKY WINTERS ZIARANI MKOANI ARUSHA

Senator JACKY WINTERS wa jimbo la OREGON MAREKANI (katikati pichani) akicheza ngoma ya asili katika ziara yake kwenye kituo cha kulelea watoto Yatima wakati wa ziara yake ya kutembelea vituo vinavyosimamiwa na shirika la ORPHANS FOUNDATION, mkoani ARUSHA
SENATOR JACKY akiendelea kuisakata ngoma akipewa kampan na mwenyekiti wa ORPHANS FOUNDATION
SENATOR JACKY akilipia mavazi ya kimasai aliyonunua
Baadhi ya wageni walioongozana na SENATOR JACKY wakichaguaa baadhi ya vitu vya asili vilivyokuwa vikiuzwa na akinamama wajane wanaosimamiwa na shirika hilo la ORPHANS FOUNDATION...
                                               PICHA Kwa hisani ya Issa Michuzi

HAPPY BIRTDAY 2ME

Jamani leo ni Siku yangu muhimu na ya historia kwa Familia ya bwana na marehemu bibi YUNUS MOHAMED kwa kuwa siku kama ya leo miaka kadhaa iliyopita ndipo nilizaliwa mimi.. Naomba kuchukua nafasi hii kuwashukuru wazazi wangu kwa kunileta hapa duniani na kunilea katika maadili mema ambayo yamenijenga na kunifikisha hapa nilipo.. Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema ahsante sana wazazi wangu na ninawapenda sana, lakini nasikitika pia kuifurahia siku hii bila ya mama yangu ambae ndiye alikuwa msingi mkuu wa maisha yangu katika kila hatua niliyoipitia kwa kuwa sasa hatuko naye tena duniani ametangulia mbele za haki... MAMA nakuombea kila kukicha MWENYEZIMUNGU AIWEKE ROHO YAKO MAHALI PEMA PEPONI, AMINA
Nilipofika ofisini watu wengi walinipongeza na tukapiga picha za ukumbusho kama unavyoona(hapo juu nikiwa nimepozi na HALIMA FRED Producer wa SKOOOOOONGAAAAAA)

Mutoto muzuri na BASILISA JOHN Presenter wa ujenzi 


             Jamani sitokuwa na fadhila nisipomshukuru MUPENZI sababu yeye ndo alinikumbusha kuwa leo ni siku yangu ya kuzaliwa maana mwenyewe mambo mengi na nilishasahau kabisaaaa, nikashangaa naambiwa ukifika Posta nisubiri baada ya kukutana naambiwa Hapi b'day bby nikasenma loh kumbe ndo tarehe 20 imeshafika hivyooo... lol!!! Thanx much baby.... LUV UUUUUUUUUU.

Tuesday, July 19, 2011

MANYWELE KIMWANA WA TWANGAPEPETA 2011 "MARY KHAMIS" KUZIBA PENGO LA AISHA MADINDA

MARY KHAMIS (katikati) akiwa na mshindi wa pili wa shindano (kushoto) na pamoja na mshindi wa tatu



AISHA MADINDA akiwa na Mkurugenzi wa EXTRA BONGO, ALLY CHOKI

Muda mfupi baada ya Mnenguaji mahiri bongo AISHA MADINDA kuihama Bendi yake ya Twanga Pepeta na kutimkia Extra Bongo, Mkurugenzi wa Twanga pepeta ASHA BARAKA amemtangaza MARY KHAMIS mshindi wa Manywele kimwana wa Twanga Pepeta 2011 kuziba pengo hili lililoachwa na AISHA, ASHA BARAKA amesema uamuzi wa kumchukua MARY umekuja baada ya kuvutiwa na kuridhishwa na umahiri alioufanya Kimwana huo wakati wa shindano hilo na hatimaye kuibuka mshindi... Wakati huohuo Mkurugenzi wa Extra Bongo ALLY CHOKI jana amemtambulisha rasmi AISHA MADINDA kuwa ni mnenguaji mpya wa bendi yake hiyo


Monday, July 18, 2011

JENNIFER LOPEZ "J.LO" NA MARC ANTHONY WAVUNJA NDOA YAO

Baada ya ndoa yao kudumu kwa muda wa miaka saba, Mwanamuziki JENNIFER LOPEZ maarufu kama J.LO na mume wake ambae pia ni mwanamuziki na muigizaji MARC ANTHONY sasa ndoa hiyo imefikia tamati

J.LO na MARC ANTHON ambao walifunga ndoa June 2004 na kubahatika kupata watoto wawili mapacha MAX na EMME wenye umri wa miaka mitatu, kila mmoja kwa upande wake amekiri kuwa pamoja na kwamba uamuzi wa kutengana ni mgumu na unaoumiza sana lakini inapobidi kila mmoja anapaswa kuheshimu maamuzi ya mwingine kama walivyofanya wao.

EPIC NATION YA EATV NA ZANTEL YAFUNIKA- MWEMBEYANGA

Mtoto wa nyumbani JUMA NATURE akipagawisha mashabiki

Umati wa watu uliofurika siku hiyo

Akiwakilisha  Ilala CHIDY BENZ na CHIKU KETO

CHIDY BENZ baada ya mzuka kupanda ilibidi avue shati


Mzee YUSUPH nae akirusha juu vidole vya mashabiki
Mashombeshombe NURU na BOB JUNIOR the PREZDAA




Ulinzi na Usalama wetu ndio kila kitu kama tunavyoona picha yenyewe inajieleza

Friday, July 15, 2011

NURU MBIONI KUTOA ALBUM YAKE

Baada ya kutoka na ngoma yake MUHOGO ANDAZI ambayo inakimbiza katika vituo mbalimbali vya Redio na Televisheni hapa Bongo akiwa amemshirikisha BOB JUNIOR,  Mwanamuziki wa Kizazi kipya NURU (Pichani) amesema kwa sasa anajipanga ili aweze kutoa Album yake mwishoni mwa mwaka huu.

Akizungumza na E-NEWS ya EATV, NURU amesema mpaka sasa tayari ngoma sita zimekwishakamilika anachosubiri kwa sasa ni kukamilisha ngoma zilizosalia ili kukamilisha Album hiyo ambayo itakuwa na nyimbo kumi katika Ladha tofauti tofauti, ambayo amepanga kuidondosha mwishoni mwa mwaka huu.

LINEX ANAKUJA NA SINA NGEKEWA

Baada ya kuteka soko la Burudani kwa ngoma zake "Mama Halima" na "Moyo wa Subira", Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya BONGO FLAVA (LINEX) anatarajia kutoa ngoma yake mpya inayoitwa SINA NGEKEWA.. LINEX amesema wimbo huo ambao umetengenezwa na Producer C9 kutoka KIRI RECORDS unatarajiwa kutoka mwanzoni mwa mwezi wa nane.. LINEX ameongeza kuwa wimbo huo ni muendelezo wa Album yake ya pili ambapo wiki moja mara baada ya ngoma hiyo kutoka ataachia na Video yake.

PARTY YA PONGEZI KWA YANGA NYUMBANI LOUNGE- ILINOGAJEEE???

Jide muandaaji wa Party hiyo katika Picha ya pamoja na Wana Yanga

Nsajigwa Team Captain akishuhudia kinywaji kinavyomiminwa, inaonyesha anakitamani mwenyewee

Hongera ASAMOAH kwa kutupatia ushindi, na hii ndiyo zawadi yako kaka


Mlezi wa Yanga FRANCIS KIFUKWE na wana Yanga wengine

Hiyo si kandambili kama unavyoionaa ni Cake hiyo, mambo ya ubunifu tuuu ya JIDE hayo

Mwenyekiti akinena jambo hapo wakati MR & MRS kwa pembeni wakifuatilia kwa umakini

MR & MRS wakiwajibika hapo na kitu cha Champaigne

Upande wa Film Industry nao walikuwepo kuwakilisha lakini sina hakika km nao ni wana yanga au vp!!!

Baada ya yote hayo burudani ilifuata kama ambavyo unaona hapo picha inajieleza.... PICHA kwa HISANI ya JAYDEE