Mbunge mteule wa Arumeru mashariki(CHADEMA), Joshua Nassari (Kushoto) na mpinzani wake Sioi Sumari wa CCM. |
MGOMBEA Ubenge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amewashinda wagombea wenzake saba kutoka vyama vya CCM, AFP, DP, NRA, SAU, UPDP na TLP katika uchaguzi mdogo wa Ubunge uliofanyika Aprili 1, 2012.
Kwa Mujibu wa Matokeo ya liyotangazwa asubuhi hii yanaonesha kuwa Mgombea Ubunge wa 32,97226,757.
Mkurugenzi wa Wilaya ya Arumeru Bw. Gracias Kagenzi amemtangaza mgombea wa CHADEMA Bw. Joshua Nassari kuwa mshindi.
Kagenzi pia ametangaza matokeo ya wagombea wengine ambao walitoka vyama vingine vya Siasa nchini kama yafuatavyo:-
AFP – 139, DP -77, NRA – 35, SAU – 22, UPDB – 18 na TLP – 18.
Kwa mujibu wa Bw Kagenzi zaidi ya watu 120,000 walijiandikisha na waliojitokeza kupiga kura walikuwa 60,696 ambapo kura halali zilikuwa 60,038 na zilizoharibika ni kura 661.
Wakati huohuo katika uchaguzi wa Udiwani uliofanyika jana CHADEMA imepata Ushindi katika Kata za Kirumba mkoani Mwanza na Kiwira mkoani Mbeya.
No comments:
Post a Comment