Tuesday, April 3, 2012

NAJUA NAWADATISHA MASHABIKI HASA WANAUME LAKINI HII NDO STYLE YANGU: ASEMA SHILOLE

Shilole kazini

Shilole katika pozi
Msanii wa filamu ambae kwa sasa ameibukia kwenye soko la muziki Bongo, Shilole ameweka wazi kuwa anajua kuwa style yake ya uchezaji wa kukatika inawadatisha sana mashabiki wake hasa kwa upande wa wanaume lakini hawezi kuiacha style hiyo kwa kuwa ndiyo style aliyoichagua na ndiyo inamuongezea mashabiki.

Akizungumza na Blog hii leo mchana Shilole amefunguka kuwa anajua kuwa mashabiki wanachanganyikiwa sana na style yake hiyo hasa kwa wanaume wenye uchu wa wanawake lakini hiyo itabaki kuwa style yake na hajali kwa kuwa anaamini kukatika ni moja ya sifa za mwanamke wa kiafrika.

Akizungumzia muziki wake Shilole amesema kuwa pamoja na kwamba ametoka na ngoma kadhaa za style ya mduara lakini anaweza kufanya aina tofauti ya muziki na kwa kudhihirisha hilo amejipanga kwa ajili ya ngoma yake mpya atakayomshirikisha Tunda man ambayo ni aina ya chakacha akaongeza kuwa studio na jina la wimbo atawafahamisha mashabiki wake mara baada ya ngoma hiyo kukamilika.

No comments:

Post a Comment