Wednesday, April 4, 2012

MASHAUZI CLASSIC NA TWANGA PEPETA KUTOA BURUDANI UTAMBULISHO WA WASHIRIKI WA MISS TABATA

Mashauzi Classic wakiongozwa na Isha Mashauzi
Baadhi ya Wanenguaji wa African Stars band (Twanga pepeta)

 
 Bendi za African Stars “Twanga Pepeta” na Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” (Pichani) wanatarajiwa kutumbuiza kwenye onyesho la utambulisho wa Miss Tabata 2012 siku ya Pasaka katika ukumbi wa Dar Wes Park, Tabata.
 
Akizungumza na blog hii Mratibu wa shindano hilo Godfrey Kalinga amesema kuwa bendi hizo mbili zitafanya maonyesho yao kabla ya warembo kutambulishwa na hata baada ya utambulisho zitaendelea kutoa burudani kali hadi majogo huku wapenzi wao wakisherehekea sikukuu ya Pasaka.

Kalinga amesema onyesho hilo maalum ambalo limeandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts chini ya udhamini wa Konyagi litakuwa ni onyesho maalum kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Pasaka na kutambulisha warembo watakaoshiriki kwenye shindano la kumsaka Miss Tabata 2012 ambalo limepangwa kufanyika mwezi ujao.

Ameongeza kuwa wakati wapenzi wa muziki wa Taarab na Dansi wakipata burudani kutoka katika Bendi hizo mbili nao mashabiki wa mambo ya urembo pia siku hiyo watapata fursa ya kuwaona warembo hao kabla ya kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni mwa Mei. 
 
Mratibu huyo amesema warembo wanaotarajia kushiriki kwenye shindano hilo la Miss Tabata wanaendelea na mazoezi katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata chini ya wakufunzi watatu - Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo Junior. 

Aidha amewataja Warembo hao kuwa ni  Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin  (19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).

Wengine ni  Neema Innocent (19), Ellen Sule (22),  Wiklihemina Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21), Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19).  
Warembo hao zaidi ya 10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala,  Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo anayeshikilia taji la Tabata ni  Faiza Ally.

No comments:

Post a Comment