Thursday, April 5, 2012

BREKING NEWS: MAHAKAMA KUU KANDA YA ARUSHA YAMVUA UBUNGE GODBLESS LEMA

Godbless Lema akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuvuliwa ubunge


Mahakama kuu ya Mkoa wa Arusha imemvua ubunge aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha mjini kwa Tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema mapema leo asubuhi kutokana na kesi ya kupinga matokeo iliyokuwa imefunguliwa dhidi yake (Godbless Lema) iliyokuwa ikiendelea mkoani humo.

Hukumu hiyo imefikiwa leo 05.04.2012 asubuhi mbele ya Jaji mfawidhi wa kanda ya sumbawanga Gabriel Rwakibarila katika hukumu ya kesi ya kupinga matokeo ya ubunge Jimbo la Arusha yaliyowasilishwa na wanachama watatu wa Chama cha mapinduzi (CCM) ambao ni Mussa mkanga(55), Agness Mollel (44) na Happy Kivuyo(49) waliotaka mahakama kuu kutengua ushindi wa Mbunge huyo kwa madai kuwa Mshindi(Godbless Lema) alitumia za kashfa, matusi na kejeli katika mikutano ya kampeni aliyoifanya wakati wa uchaguzi jimboni humo.

No comments:

Post a Comment