Monday, April 23, 2012

RAY KUMBURUZA MAHAKAMANI MMILIKI WA U-TURN BLOG

 Kifo cha Nguli wa Filamu nchini, Steven Kanumba kimeibua mjadala mpya baada ya nyota mwingine wa filamu nchini Vicent Kigosi(Pichani juu) kuibuka na kusema kuwa atahakikisha anamfikisha mahakamani mwanadada Mange Kimambi (pichani chini)kwa madai kuwa amemtuhumu kupitia Blog yake ya U turn kuwa naye(Ray) ni mhusika wa kifo hicho cha muigizaji mwenzake Steven Kanumba.

Mange Kimambi(Mmiliki wa U turn Blog)
Akizungumza na Radio moja jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki Ray alifunguka kuwa mwanadada huyo ambaye hata hamfahamu aliandika kwenye blog yake kuwa "aliyemuua Kanumba siyo muigizaji Elizabeth Michael "Lulu" aliyeko mahabusu hivi sasa ila mhusika hasa ni Ray na kuongeza kuwa Ray huyo huyo ndiye aliyempigia simu Lulu wakati akiwa nyumbani kwa Steven Kanumba na kupelekea ugomvi ambao inasemekana kuwa ndiyo ulisababisha kifo chake(Steven Kanumba)

Ray ameongeza kuwa hatolifumbia macho suala hili kwa kuwa limemdhalilisha na kumvunjia heshima sana mbele ya mashabiki wake na wapenzi wakehata hivyo suala hilo limemjengea picha mbaya kwa mashabiki hao na litamharibia hata kazi yake ya uigizaji ambayo ndiyo anaitegemea katika kuendesha maisha yake.

Angalizo: Naomba kutoa angalizo kwa wamiliki wa vyombo vya habari hasa hizi Blog, wengi wao wamekuwa wakizitumia vibaya kwa kuandika mambo ambayo hawana hata uhakika nayo bila hata kufikiria athari za pande zote mbili kwake mwandishi lakini hata huyo anayeandikwa kama ambavyo amefanya Mange bila hata ya kufikiri, hii ni hatari inabidi tuzingatie maadili ya vyombo vya habari tunapoandika habari zetu, tusikurupuke tu kwa kuwa tumesikia.

No comments:

Post a Comment