Wednesday, April 11, 2012

MAMA MZAZI WA ELIZABETH MICHAEL(LULU) AZUNGUMZA KUHUSU KESI INAYOMKABILI MWANAE

Mama mzazi wa muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya mcheza Filamu mwenzake Steven Kanumba, amezungumzia namna alivyoguswa na kifo hicho na kuyaomba mashirika yanayotetea haki za binadamu wamsaidie katika kesi ya mtoto wake ili kuhakikisha haki inatendeka.

Akizungumza na kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kila Jumanne kupitia EATV, amesema kuwa yeye kama mzazi ameguswa sana na kifo cha marehemu Steven Kanumba ambae alikuwa ni mwanae pia lakini ametumia nafasi hiyo kumpa pole mzazi mwenzie, mama mzazi wa marehemu.

Aidha mama huyo amewaomba waandishi wa habari kutoegemea upande mmoja wala kuhukumu wanapoandika habari zao na kuwataka wasubiri uamuzi wa mahakama kwa kuwa kesi hiyo tayari ipo mahakamani.

Katika hatua nyingine amewaomba wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamsaidie katika kesi ya mwanae ili haki itendeke katika maamuzi ya mahakama.

No comments:

Post a Comment