Thursday, April 5, 2012

SI BURE UNA MAPUNGUFU YA MASHAUZI CLASSIC KUZINDULIWA MKESHA WA PASAKA


Kundi jipya la muziki wa Taarab linalokuja juu nchini, Mashauzi Classic linatarajia kuzindua Album yake ya kwanza jumamosi ya mkesha wa pasaka katika ukumbi wa Travertine Hotel magomeni, jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Blog hii Mkurugenzi wa kundi hilo Isha Ramadhani a.k.a Isha mashauzi amesema, Album hiyo yenye nyimbo tano inakwenda kwa jina la "Si bure una mapungufu".

Amezitaja nyimbo hizo tano na waimbaji wake kuwa ni, "Si bure una mapungufu" wimbo ambao umebeba jina la album umeimbwa na yeye mwenyewe(Isha), "Anayejishuku hajiamini" umeimbwa na mdogo wake Saida Ramadhani, "Niacheni nimpende" muimbaji ni Hasheem said, "mdomo wako utakuponza" umeimbwa na Fatma Seif na wimbo wa tano na wa mwisho ni "Fungu la kukosa"

Isha ameongeza kuwa lengo la Album hiyo yenye nyimbo tano ambazo zote zimetungwa na Thabit Abdul ilitakiwa kuwa na nyimbo nne lakini waliongeza wimbo wa tano kama zawadi kwa mashabiki wao.

Uzinduzi huo wa Album ya kwanza ya mashauzi Classic utasindikizwa na kundi la Coast modern Taarab wakiongozwa na Omary Tego pamoja na Barnaba boy kutoka THT.

No comments:

Post a Comment