Tuesday, April 3, 2012

ALICHOKISEMA WEMA KUHUSU DIAMOND KUKATAA PESA ZAKE DIAMONDS ARE FOREVER

Wema kwenye show ya Diamonds are Forever
Mengi yamezungumzwa kuhusiana na tukio la mwanamuziki Diamond kukataa pesa za aliyekuwa mchumba wake Wema Abraham Sepetu pale alipokwenda kumtuza mkali huyo wa Bongo fleva stejini, hatimaye jana Wema mwenyewe amefungua mdomo kuhusu tukio hilo.

Akizungumza na Radio moja jijini Dar es salaam, Wema amesema amejisikia vibaya kutokana na tukio hilo lakini hakuna jinsi kwa tayari limeshatokea ila kwa upande wake amekichukulia kitendo hicho kama ni ushamba na uswahili na kuahidi kuwa atazidi kuwa shabiki wake na ataendelea kumsupport ila abadili tabia.

Aidha Wema ameongeza kuwa pamoja na kuachana kwao lakini hawapaswi kuwa maadui na alimpelekea pesa kwa kuwa anaupenda sana wimbo wa mawazo ambao ulikuwa ukipigwa wakati huo na ndiyo maana alinyanyuka na kwenda kumpa pesa.

 Kuhusu hisia za kimapenzi, Wema amesema kwa sasa hana hisia zozote za kimapenzi na Diamond na hayuko tayari hata kuanza naye ukurasa mpya.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya Diamond kuwa Wema anajitafutia umaarufu kupitia jina lake, amemshangaa sana Diamond na kusema"Mimi nimekuwa staa tangu 2006 yeye amneanza kujulikana mwaka 2010, pliz Diamond umenidisapoint sana, jirekebishe.

No comments:

Post a Comment