Tuesday, April 3, 2012

CCM WAKUBALI MATOKEO YA UBUNGE ARUMERU





katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa  ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye (pichani) amesema wanawapongeza CHADEMA kwa ushindi walioupata katika viti mbalimbali ikiwemo Ubunge wa Arumeru mashariki na Udiwani katika baadhi ya kata na  wanampongeza Nassari na kutoa wito "ikiwa yeye kama kijana ajitahidi kusukuma kwa kuhakikisha yale aliyoahidi yanatekelezeka ili watanzania waendelee kuwaamini vijana, sisi kama Chama tumepokea kwamba tumefanya kampeni kwa siku zote lakini wananchi wa Arumeru wamewachagua wao na sisi tumelipokea kwa mikono miwili kwamba ndio sauti ya wana Arumeru”

Nnauye ameongeza zaidi kuwa “tumekubaliana na matokeo na ndio maana tumechukua hatua ya kuwapongeza, sasa maneno mengine yote yatakayosemwa ni maoni ya watu lakini msimamo wa chama chetu ni kwamba tunataka tuue dhana ya kwamba uchaguzi ambao ni huru na haki ni ule ambao wewe umeshinda, usiposhinda basi haukua huru na wa haki, sisi hatuamini katika hilo akaongeza kuwa tunaamini kwamba asiekubali kushindwa sio mshindani kwa hiyo sisi tumekubali, inawezekana tuliteleza mahali au mbinu za mikakati uwanjani walituzidi wenzetu ndio maana wameshinda, tumekubali na tunawatakia kila la kheri”. Alisema Nape alipozungumza na waandishi wa habari.



No comments:

Post a Comment