Thursday, April 5, 2012

BAADA YA WEMA KUFUNGUKA KUHUSU DIAMOND KUKATAA PESA ZAKE DIAMOND NAE AJIBU MAPIGO


Baada ya Miss Tanzania 2006 ambae pia ni bongo movie star Wema Sepetu kuzungumza na Radio moja jijini DSM kwamba alichokifanya Diamond kukataa kuchukua pesa yake ni uswahili, Diamond nae ameamua kuzungumza na millardayo.com

Kabla ya kukupa alichosema Diamond, Wema alikanusha pia kuhusu stori kwamba alikwenda nyumbani anapoishi Diamond ili waondoke wote kwenda kwenye show Mlimani City kwa kuthibitisha kwamba hapajui hata Diamond anapoishi.

Baada ya kukasirishwa na alichokisema  Wema, Diamond aliomba kuzungumza na Radio hiyo na kukiri kwamba “kiukweli mimi sipendi ugomvi, na haya nisinge yasema kama yeye asingekuja kuongea uongo, yani hata sababu kubwa ya mimi na yeye kutofautiana ilikua ni kitu kidogo tu anakipeleka kwenye media na ikafika time anasema hanitaki ila mimi ndio namng’anga’nia wakati ukweli ni kwamba alikua analetwa nyumbani na rafiki zake na ndugu zake akilia anaomba isuluishwe turudiane, mpaka anampigia mama yangu mzazi, rafiki zangu na ndugu kama Shetta na Romy Jones, pia anawaambia marafiki zake waandae sehemu ya Dinner ili atokee kama Suprise”

Diamond amesema “kabla ya show yangu ya juzi alikuja nyumbani mimi niko ndani navaa nasikia sauti yake barazani, namuuliza ndugu yangu Rommy ananiambia ni Wema, nauliza kafata nini nyumbani? mimi nina mpenzi wangu na yeye anamfahamu na hizi drama za Wema zinafanya mpenzi wangu akasirike kwa sababu anaona bado naendelea na Wema, sasa pale nyumbani nilitoka nje baada ya kukasirika ila wakanishika nisimguse, ndio wakamwambia aondoke… yani baada ya kugundua kwamba mimi sitaki kuwa na yeye tena sasa anatumia kama ile ha
taki kuwa na mimi, Nakuharibia sasa”

“Wakati anakuja kunipa hela kwenye stage mi nilikua naogopa kwa sababu tayari alikuja nyumbani kabla yake ndio maana nilihisi anataka kufanya drama nyingine tena ndio maana nikamkwepa na kujifanya kama sijamuona lakini akaganda makusudi kama anataka kufanya kitu flani, mpaka mwisho baadae akamfata Q Chief anamlilia pia kawafata mama yangu na mama mdogo anawaambia mimi mtoto wenu nampenda sana ananitesa, halafu baada ya hapo anakuja kwenye Media na kuongea vitu vingine, na kunitengenezea mazingira ili mimi nionekane mbaya” – alisema Diamond

Katika sentensi nyingine Diamond amethibitisha kwamba kwenye  hiyo show yake kulikuwa na wasichana wawili ambao waliwahi kuwa wapenzi wake, na walijitokeza pale kwenye stage na kumpa pesa na yeye alizipokea bila tatizo kwa sababu hana tatizo nao akiwemo Sarah ambae alimwimbia “Nenda kamwambie” ila za Wema alizikataa makusudi kwa sababu alikuwa anataka kutengeneza drama manake ishu isingeishia pale.



 

No comments:

Post a Comment