Friday, March 30, 2012

MABALOZI WA NCHI TISA WATEMBELEA MKOA WA MTWARA

MABALOZI tisa wa Umoja wa Ulaya pamoja na mwenzao kutoka Norway walitembelea mkoa wa Mtwara ambapo walifanya mazungumzo na wadau wa maendeleo kuhusu mambo mbali mbali yahusuyo mkoa huo pamoja na shughuli na matarajio ya baadae katika sekta ya gesi asilia.

Ziara hiyo iliongozwa na Balozi Filiberto Ceriani Sebregondi, ambaye ni mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa Tanzania, ambaye pia alikuwa mwenyekiti wa kundi hilo. Ilijumuisha wanadiplomasia kutoka katika balozi zilizopo Tanzania za nchi za Ubelgiji, Denmark, Finland, Ufaransa, Ujerumani, Hispania, Sweden na Uingereza. Balozi wa Norway pia alishiriki pia katika ziara hiyo.

Wakuu hao wa balozi za nchi zao hapa Tanzania walitembelea Bandari ya Mtwara, Kisima cha kuchunguza uwepo wa mafuta baharini, mtambo wa kutengeneza gesi na mtambo wa kuzalisha nishati kwa kutumia gesi uliopo jirani na bandari hiyo. Pia walifanya mikutano na maofisa wa serikali mkoani humo akiwemo Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bi. Hasna Mwilima, na wadau wengine.

No comments:

Post a Comment