Tuesday, April 3, 2012

NIMEIPENDA SANA HII: NI MAKUZI NA MAZOEA YANAYOENDESHA NDOA YAKO

Hapo awali nilipata kuandika kuhusu NDOA vs HARUSI ambapo nilieleza lile ninaloamini kuwa "Mahusiano yake ni madogo sana (kama yapo) na pia mafanikio ya moja kati ya hayo hayana AKISI ya moja kwa moja kwa jingine. Tofauti baina yake ni kubwa kuliko inavyochukuliwa na umuhimu wa elimu juu ya uelewa wake ni zaidi ya inayotolewa.
Nilielezwa kuwa HARUSI ZOTE ZAFANANA JAPO KILA NDOA NI YA KIPEKEE. Na kuwa waweza kuwa na ndoa bila harusi na harusi isiyo na ndoa ya kweli."
Kisha nikarejea kwenye SWALI LA MSINGI kuwa "Kwanini tuwe na NDOA na HARUSI kama uhusiano wake waweza kutomaanisha lolote kwa pamoja?"
Lakini kabla ya NDOA na hata HARUSI kunakuwa na MAZOEA YANAYOTOKANA NA MAKUZI tuliyokuzwa kabla hatujakutana na "asali wa moyo" wetu. Na haya yana nafasi kubwa saana katika maisha yetu.
Ni wazi kuwa jamii nyingi za kiAfrika zimejengwa ama kujijenga kwenye mfumo ambao MWANAUME NI KICHWA CHA FAMILIA. Na hili linaifanya jamii iwaone wanawake kama "daraja la pili" katika familia.
Na ndio maana hata inapotokea mwanaume akafanya baadhi ya mambo "yasiyokubalika", anaweza kuonekana kama anafanya "jambo la kiume" ilhali jambo hilo likitendwa na mwanamke, itaonekana KITUKO.
Mfano mdogo ni ULEVI. Kwa mwanaume kulewa mpaka kesho yake akaokotwa mtaroni yaweza kuwa "uanaume" ilhali mwanamke akilewa akawa anaanguka na kuamka mpaka akafika kwake, anaweza kuwa "gumzo la mtaa".
 
Kujifunza mengi zaidi zama hapa

2 comments:

  1. ni kweli hili ni darsa kabisa...Nimepita kukusalimu kwa leo nimekukutata kwa Mzee wa changamoto.

    ReplyDelete
  2. Ooh!Ahsante kwa kutembelea mitaa hii, karibu tena na tena.

    ReplyDelete