Wednesday, April 11, 2012

ELIZABETH MICHAEL(LULU) AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Nyota wa Filamu nchini anayeshukiwa kuhusika na kifo cha mcheza Filamu Steven Kanumba Elizabeth Michael(Lulu) amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam ili kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Nyota huyo wa filamu aliyefariki April 7 na kuzikwa janaApril 10 katika makaburi ya kinondoni.

Amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Augustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ambapo kesi yake imeahirishwa mpaka Tarehe 23.04.2012 na mtuhumiwa kupelekwa katika gereza la segerea.

Katika kesi hiyo Elizabeth hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi mauaji.

Wakati huohuo kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi kinondoni, Charles Kenyela amesema umri wa muigizaji huyo nyota ni tofauti na ule alioandikisha katika maelezo yake.

Kamanda Kenyela ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio leo mchana ambapo amesema amekiona cheti cha Lulu lakini umri aliouandika katika maelezo yake hauendani na ule uliopo kwenye Cheti chake, na alipoulizwa kuhusu umri kamili wa msanii huyo alisema hakumbuki kila kitu ila anachokumbuka ni kuwa umri aliousema wa miaka 18 (Kumi na nane) ni tofauti na uliopo kwenye cheti chake cha kuzaliwa.

Hata hivyo habari zilizoifikia Blog hii kutoka kwa mtu wa karibu na Lulu zinasema kuwa msanii huyo anatimiza umri wa miaka 17(kumi na saba) ifikapo Tarehe 16.04.2012.  

kufahamu zaidi kuhusiana na kesi hiyo endelea kufuatilia Blog hii.

No comments:

Post a Comment