Monday, April 23, 2012

MASHUJAA MUSICA YAZIDI KUIBOMOA TWANGA, WALETA MZIGO MPYA KUTOKA EXTRA BONGO

Bendi ya muziki wa dansi nchini, Mashujaa musica iliyokuja na style ya kukomba wanamuziki kutoka katika Bendi mbalimbali nchini, baada ya kuivuruga Bendi kongwe ya Twanga Pepeta  na kuchukua wanamuziki wake tegemezi kama Charles Baba na Lilyan Internet imeendeleza vurugu zake kwa Bendi hiyo ambapo sasa imetangaza kumnyakua Mpiga Drums tegemezi wa Bendi hiyo maarufu kama MCD (pichani juu)
Akizungumza na Blog hii mkurugenzi wa bendi hiyo Max Luhanga akiwa njiani kuelekea Morogoro kwa shughuli za kikazi amesema, bado wanaendelea na mchakato wa kuimarisha bendi yao ambapo pia wamemchukua Rapa maarufu wa Bendi ya Extra Bongo anayefahamika kwa jina maarufu la Ferguson (pichani), na kuongeza kuwa kila kitu kimeshakamilika kilichobaki ni kusubiri utambulisho rasmi ambao utafanyika Ijumaa ya April 27 katika ukumbi wa Business park uliopo Victoria jijini Dar es salaam.. Kaa kushuhudia uzinduzi huo kupitia Afrobeat ya Eatv, Stay tuned.



RAY KUMBURUZA MAHAKAMANI MMILIKI WA U-TURN BLOG

 Kifo cha Nguli wa Filamu nchini, Steven Kanumba kimeibua mjadala mpya baada ya nyota mwingine wa filamu nchini Vicent Kigosi(Pichani juu) kuibuka na kusema kuwa atahakikisha anamfikisha mahakamani mwanadada Mange Kimambi (pichani chini)kwa madai kuwa amemtuhumu kupitia Blog yake ya U turn kuwa naye(Ray) ni mhusika wa kifo hicho cha muigizaji mwenzake Steven Kanumba.

Mange Kimambi(Mmiliki wa U turn Blog)
Akizungumza na Radio moja jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki Ray alifunguka kuwa mwanadada huyo ambaye hata hamfahamu aliandika kwenye blog yake kuwa "aliyemuua Kanumba siyo muigizaji Elizabeth Michael "Lulu" aliyeko mahabusu hivi sasa ila mhusika hasa ni Ray na kuongeza kuwa Ray huyo huyo ndiye aliyempigia simu Lulu wakati akiwa nyumbani kwa Steven Kanumba na kupelekea ugomvi ambao inasemekana kuwa ndiyo ulisababisha kifo chake(Steven Kanumba)

Ray ameongeza kuwa hatolifumbia macho suala hili kwa kuwa limemdhalilisha na kumvunjia heshima sana mbele ya mashabiki wake na wapenzi wakehata hivyo suala hilo limemjengea picha mbaya kwa mashabiki hao na litamharibia hata kazi yake ya uigizaji ambayo ndiyo anaitegemea katika kuendesha maisha yake.

Angalizo: Naomba kutoa angalizo kwa wamiliki wa vyombo vya habari hasa hizi Blog, wengi wao wamekuwa wakizitumia vibaya kwa kuandika mambo ambayo hawana hata uhakika nayo bila hata kufikiria athari za pande zote mbili kwake mwandishi lakini hata huyo anayeandikwa kama ambavyo amefanya Mange bila hata ya kufikiri, hii ni hatari inabidi tuzingatie maadili ya vyombo vya habari tunapoandika habari zetu, tusikurupuke tu kwa kuwa tumesikia.

JACOB ZUMA AVUTA JIKO LA SITA

Wakati wa ndoa ya kimila, Zuma akiwa amevaa ngozi ya chui huku amebeba ngao
Wakikata keki baada ya ndoa yao
Zuma na mkewe (Bongi ngema) wakiwa na nyuso za furaha wakati wa ndoa yao

Source:





Thursday, April 19, 2012

TWANGA PEPETA YAMNYAKUA BADI BAKULE


Muda mfupi baada ya Bendi ya Levent Musica iliyokuwa na makazi yake mjinimorogoro kusambaratika, Mmoja kati ya waimbaji wake Badi Bakule (pichani) amerejea jijini Dar es Salaam na kujiunga na Bendi ya African Stars (Twanga pepeta).

Meneja wa Bendi hiyo Hassan Rehani amesema mwimbaji huyo amejiunga na Bendi hiyo mwanzoni mwa wiki hii na wanatarajia kuanza kumtambulisha Rasmi Kesho Ijumaa katika ukumbi wa Africenter-Ilala na baadae watafanya utambulisho mwingine siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Mango garden Kinondoni.

Rehan ameongeza kuwa wamemchukua Badi Bakule kutokana na uwezo wake katikautungaji na uimbaji ambapo ameziba pengo la muimbaji wa sauti ya tatu ambayo haina mwimbaji wa kutegemewa.

Mengi zaidi kuhusiana na Badi Bakule kuhamia Twanga pepeta utayapata kupitia Afrobeat wiki ijayo.... Usikoseeeeeeeee!!!!

Wednesday, April 18, 2012

HAWA NDIYO WABUNGE WA BUNGE LA AFRIKAMASHARIKI

Mh.Makongoro Nyerere

Mh. Shy-Rose Bhanji

Mh. Angella Charles Kizigha
Pichani juu ni kati ya wabunge Tisa wa Bunge la Afrika Mashariki waliochaguliwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania, katika ukumbi wa Bunge Dodoma jana.

Wabunge wengine waliochaguliwa jana ni pamoja na Mwinyi Hassan, Taslim Twaha Issa,Kesi Ndelakindo Prepetua, Kimbisa Adam Omary, Yahya na Murunya Bernard.

Blog hii inawapongeza wale wote waliopata ushindi huo lakini pia inawatakia kila la kheri wale wote waliojaribu lakini kura hazikutosha na kuwatia moyo kuwa wasikate tamaa na wajaribu wakati mwingine.

Tuesday, April 17, 2012

WASHINDI WA TUZO ZA KILIMANJARO 2012 KUFANYA ZIARA MIKOANI

Afisa masoko wa Eatv Olympia Fraten akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara waliyoiandaa kwa ajili ya washindi wa Tuzo za Kilimanjaro 2012 katika mikoa mbalimbali nchini, ambapo amefafanua kuwa Eatv pekee itakuwa ikirusha ziara nzima ya wasanii hao.

Meneja masoko wa Bia ya kilimanjaro, George Kavishe(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ziara ya washindi wa Tuzo za kilimanjaro(Kilimanjaro Tanzania music Awards 2012) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Savannah Lounge jijini Dar es salaam kushoto ni Afisa masoko wa Eatv Olympia Fraten ambao ni waratibu wa ziara hiyo na kulia ni mmoja wa washindi wa Tuzo hizo Naseeb Abdul(Diamond)

Sunday, April 15, 2012

KILIMANJARO MUSIC AWARDS 2012 DIAMOND ARUDI KILELENI ANYAKUA TUZO TATU

Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia nani ataondoka na nini

Washereheshaji wa usiku huo walikuwa ni Millard Ayo( kushoto) na Vanessa Mdee


Bi Shakila, Patricia Hllary kutoka Bendi ya JKT pia walikuwepo kutoa burudani usiku huo

Mpoki alituvunja mbavu zetu na kutuongezea siku za kuishi, yaani ilikuwa burudani ya kutosha sana

Queen Darleen (katikati) alijinyakulia Tuzo ya wimbo bora wa Dancehall kushoto kwake ni Taji Liundi na Kulia ni Abby waliomkabidhi Tuzo hiyo

Kushoto ni Mtangazaji mkongwe na kipenzi cha watu wengi sana Reinfred Masako kutoka ITV/Radio One na Dina Marios wa Clouds Fm wakimkabidhi Tuzo ya wimbo bora wa zouk/Rhumba mwanamuziki Ally Kiba, anayeshuhudia mwenye gauni nyeusi ni mdogo wake Ally Kiba.

Mwanamuziki AT akichukua Tuzo yake ya wimbo bora wenye vionjo vya asili aliyemsindikiza ni Mwanne aliyeshirikiana nae kwenye wimbo huo na mwenye suti ni Shelukindo na Angela Damas waliomkabidhi Tuzo hiyo

Mwanamuziki anayekuja juu kwenye muziki wa Taarab Isha Ramadhan(Mashauzi) akipokea Tuzo yake ya wimbo bora wa Taarab

Mzee Kalala kama haamini anachokisoma vileee, yuko na Shamim wa 8020 Fashions blog, wao walitoa Tuzo ya wimbo bora wa kiswahili(Bendi) Tuzo iliyoenda kwa Twanga pepeta kupitia wimbo dunia daraja utunzi wa Charles baba ambaye sasa hivi yuko Mashujaa

Malkia wa mipasho Afrika mashariki Khadija Omary Kopa, aliyenyakua Tuzo ya mtumbuizaji bora wa kike akiwa pamoja na binti zake na mume wake ambao walikuja kumpa Support usiku huo
Kiongozi wa bendi ya Twanga pepeta Luiza Mbutu akiwashukuru mashabiki kwa niaba ya Bendi
Diamond ambae amerudisha heshima yake kwa kuchukua Tuzo 3 katika Tuzo za mwaka huu baada ya mwaka jana kuambulia patupu akiwa na wapambe wake baada ya kuchukua Tuzo ya pili, mwenye gauni ya purple ni mama yake mzazi.

Thursday, April 12, 2012

SHIRIKISHO LA FILAMU NCHINI "TAFF" WAPIGA MARUFUKU UUZAJI WA VIDEO ZA MAZISHI YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake
SHIRIKISHO  la Filamu Nchini(TAFF),limesema litamchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayebainika kuuza CD za shughuli za mazishi ya marehemu Steven Kanumba bila ridhaa ya familia.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Vatican Sinza, Rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifamba alisema lengo la mkutano huo lilikuwa ni kutoa salamu za shukurani kwa wote waliohudhuria msiba huo na kutoa tahadhari hiyo.
Mwakifamba alisema tayari wameshapata taarifa za watu kuanza kuuza cd hizo kwa lengo la kujipatia fedha jambo ambalo sheria ya filamu hairuhusu.
Kwa mujibu wa Rais huyo,Kanumba alikuwa akitegemewa na familia yake kupitia kazi za filamu ambapo sasa hivi kutokana na kutokuwepo kwake familia hiyo itayumba.

Aliongeza kuwa endapo CD hizo zitaweza kusimamiwa vizuri pato lake litaingia kwenye familia na kuweza kuendesha maisha yao ya kila siku badala ya jasho hilo kufaidiwa na watu wengine.
Kwa upande mwingine Mwakifamba alisema msiba wa Kanumba ni pigo kwa tasnia ya filamu kutokana na namna msanii huyo alivyoweza kuitangaza  Tanzania kupitia kazi zake na kuongeza kuwa  TAFF itamkumbuka kwa mambo mengi,kwani mbali na kuwa mwanachama kupitia chama cha Waigizaji Kinondoni, pia alikuwa mjumbe wa kamati ya TAFF ya kuandaa mapendekezo ya marekebisho kanuni ya sheria za filamu za mwaka 2011.
Vilevile Kanumba alikuwa ni mmojawapo wa wafadhili wa Shirikisho hilo ambapo alikuwa mchango mkubwa katika kuleta umoja na mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu.

BAADA YA MAMA LULU SASA NI BABA LULU

Baba mzazi wa Elizabeth Michael "Lulu"
Baba mzazi wa muigizaji wa kike wa fialamu nchini maarufu kama Lulu, ambae anahusishwa na kifo cha marehemu Steven Charles Kanumba ameibuka na kueleza kushtushwa sana na taarifa za kifo hicho pamoja na habari kuwa bintiye alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji huyo nguli na kuhusishwa na kifo chake.

Baba Lulu ambaye alijitambulisha kwa jina la Michael Edward Kimetameta(49) mzaliwa wa wilaya ya Rombo, mkoani kilimanjaro amesema kuwa alimtambua Steven Kanumba kama mwalimu wa mwanae lakini hakuamini masikio yake pale alipopata taarifa za kifo hicho huku bintiye anayedaiwa kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu, anahusika.

Zaidi ingia hapa

TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS NI JUMAMOSI HII NDANI YA UKUMBI WA MLIMANI CITY

Kilimanjaro premium lager wanakuletea
Kilimanjaro Tanzania music awards 2012, ni jumamosi hii ya tarehe 14/04/2012 tunzo mbalimbali kutolewa kwa wasanii mbalimbali pata kujionea live Yule msanii  uliyempigia kura kupanda kwa stage na kuchukua award, huku shangwe za kutosha, good music plus performs nzito kwa wasanii nguli.
Ni mlimani city hall ndio mahala pa tukio,sh 75000/= tu kwaVIP huku ukipata buffet dinner plus drinks bureee na Tsh 20000/= kwa viti vya kawaida na BIA moja ya bure.Sasa hivi tickets zinapatikana



1. UkumbiwaMlimani city kuanzia jumatatu,
2. Posta - Baraka Garden mtaa wa Azikiwe nyuma ya CRDB Bank.
3. Zizzou Fashion ya Victoria, Sinza naTegeta.
4. Born to Shine Mwenge
5. Robbie One Fashion – Kinondoni
6. Engine Petrol Station – Mbezi.
Kilimanjaro Premium Larger, bonge la kiburudisho kwa watanzania

Wednesday, April 11, 2012

TAARIFA YA MAMLAKA YA HALI YA HEWA KWA WATANZANIA KUHUSU TSUNAMI

Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania imetoa tahadhari kuwa kutakuwa na tetemeko la ardhi(Tsunami) ambayo yanahofiwa kufika kwenye pwani ya Tanzania hasa katika maeneo ya Mkoa wa Mtwara kuanzia saa 11 jioni ya leo.

Tetemeko hilo lililotokea chini ya Bahari na kutarajiwa kutengeneza mawimbi ya Tsunami limeanzia huko Sumatra nchini Indonesia.

Aidha katika taarifa hiyo Mamlaka imewaomba wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa katika vyombo vya habari ili kufahamu hali inaendeleaje kwa kuwa watakuwa wanatoa taarifa mara kwa mara pia wamewataka wananchi wanaoishi sehemu tambarare mawimbi yanaweza kuingia ndani ila sehemu za miinuko wanaweza wasipate athari.

VICENT KIGOSI (RAY) ALIA NA WANAOMSEMA VIBAYA KUHUSU UHUSIANO WAKE NA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Mmoja kati ya wacheza filamu wakubwa nchini, Vicent Kigosi(Ray) ameezungumzia namna anavyoguswa na kuumizwa na maneno yanayosemwa na watu kuhusiana na tofauti zilizokuwepo baina yake na marehemu Steven Kanumba ambao kabla ya tofauti hizo walikuwa ni marafiki wakubwa na kufikia hatua ya kuitana "Swaiba" na pia majina ya The Great bna The Greatest" yalitokana na uswaiba huo waliokuwa nao.

Akielezea kwa uchungu namna alivyoguswa na kifo cha Swaiba wake huyo na tofauti ya yale watu wanayoyazungumza kupitia Blog yake, Ray amesema "mengi yanazungumzwa juu yangu ila kila kitu mimi namuachia Mungu mimi ni mnyonge siwezi kupambana nanyi mnaoniongelea vibaya maumivu nayoyapata juu yenu Mungu hatowaacha siwezi kuzizuia hisia zenu kuzungumza yale mnayojisikia."

Aidha Ray ameonyesha kutubu kwa yale yote yaliyotokea kati yake na Kanumba na kusema" yote yaliyotokea ni kawaida ya binadamu kutoelewana, kama Baba na Mama wanafunga ndoa kanisani na wanakula viapo vya utii mbele za Mungu lakini wanagombana na kufikia hatua ya kuachana kwanini ishindikane kwetu ni hali ya kawaida katika maisha binadamu kutofautiana.

CHUO CHA UFUNDI STADI VETA-LINDI CHAZINDULIWA RASMI


Mandhari ya jengo hilo la chuo cha ufundi stadi Veta-Lindi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.Mohamed Gharib Bilal na balozi wa Korea hapa nchini Young-Hoon Kim kwa pamoja wakikata utepe kama alama ya uzinduzi wa chuo hicho kipya cha ufundi Stadi VETA-LINDI, uliofanyika jana chuoni hapo.Kulia ni Mkurugenzi wa VETA, Zebadia Moshi.


Jiwe la msingi
Baadhi ya vifaa vitakavyotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho
Kibao cha utambulisho wa chuo hicho
Dk. Bilal akibonyeza kitufe cha alarm kuashiria uzinduzi wa chuo hicho kipya.  







MAMA MZAZI WA ELIZABETH MICHAEL(LULU) AZUNGUMZA KUHUSU KESI INAYOMKABILI MWANAE

Mama mzazi wa muigizaji Elizabeth Michael (Lulu) anayetuhumiwa kwa kesi ya mauaji ya mcheza Filamu mwenzake Steven Kanumba, amezungumzia namna alivyoguswa na kifo hicho na kuyaomba mashirika yanayotetea haki za binadamu wamsaidie katika kesi ya mtoto wake ili kuhakikisha haki inatendeka.

Akizungumza na kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa kila Jumanne kupitia EATV, amesema kuwa yeye kama mzazi ameguswa sana na kifo cha marehemu Steven Kanumba ambae alikuwa ni mwanae pia lakini ametumia nafasi hiyo kumpa pole mzazi mwenzie, mama mzazi wa marehemu.

Aidha mama huyo amewaomba waandishi wa habari kutoegemea upande mmoja wala kuhukumu wanapoandika habari zao na kuwataka wasubiri uamuzi wa mahakama kwa kuwa kesi hiyo tayari ipo mahakamani.

Katika hatua nyingine amewaomba wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wamsaidie katika kesi ya mwanae ili haki itendeke katika maamuzi ya mahakama.

TAARIFA YA POLISI KUHUSU WATU KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA MAZISHI YA STEVEN KANUMBA

Kutokana na taarifa zilizoenea mtaani kuwa kuna watu kadhaa wamepoteza maisha wakati wa mazishi ya mpendwa wetu marehemu Steven Kanumba, Jeshi la polisi limekanusha taarifa hizo.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa kipolisi Kinondoni Charles Kenyela amesema hakuna ukweli wowote wa taarifa hizo na kuwa huo ni uvumi tu uliotokana na watu wengi kudondoka, lakini ukweli ni kwamba hakuna aliyepoteza maisha.

Kenyela alibainisha kuwa wengi kati ya watu waliodondoka walipewa huduma papohapo na watoa huduma wa chama cha msalaba mwekundu(Redcross) na kupata nafuu ingawa kuna wengine walipata nafuu wakati wakiwa njiani wakipelekwa hospitali wakati watu wapatao 10 walifikishwawa Hospitali na kati yao watu 9 walipelekwa Hospitali ya mwananyamala na mmoja alipelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili na wote waliruhusiwa baada ya muda.

Kwa upande mwingine Kamanda Kenyela ameeleza kuwa pamoja na taarifa hizo pia hawajapata taarifa za watu kuibiwa ingawa idadi ya watu ilikuwa kubwa kuliko ilivyotegemewa ambapo alisema hawezi kukadiria idadi ya watu waliofika lakini kwa haraka haraka walikuwa watu zaidi ya 25,000(Elfu ishirini na tano).

ELIZABETH MICHAEL(LULU) AMEFIKISHWA MAHAKAMANI LEO

Nyota wa Filamu nchini anayeshukiwa kuhusika na kifo cha mcheza Filamu Steven Kanumba Elizabeth Michael(Lulu) amepandishwa kizimbani leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam ili kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Nyota huyo wa filamu aliyefariki April 7 na kuzikwa janaApril 10 katika makaburi ya kinondoni.

Amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Augustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ambapo kesi yake imeahirishwa mpaka Tarehe 23.04.2012 na mtuhumiwa kupelekwa katika gereza la segerea.

Katika kesi hiyo Elizabeth hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi mauaji.

Wakati huohuo kamanda wa Polisi mkoa wa kipolisi kinondoni, Charles Kenyela amesema umri wa muigizaji huyo nyota ni tofauti na ule alioandikisha katika maelezo yake.

Kamanda Kenyela ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na kipindi cha Power Jams cha East Africa Radio leo mchana ambapo amesema amekiona cheti cha Lulu lakini umri aliouandika katika maelezo yake hauendani na ule uliopo kwenye Cheti chake, na alipoulizwa kuhusu umri kamili wa msanii huyo alisema hakumbuki kila kitu ila anachokumbuka ni kuwa umri aliousema wa miaka 18 (Kumi na nane) ni tofauti na uliopo kwenye cheti chake cha kuzaliwa.

Hata hivyo habari zilizoifikia Blog hii kutoka kwa mtu wa karibu na Lulu zinasema kuwa msanii huyo anatimiza umri wa miaka 17(kumi na saba) ifikapo Tarehe 16.04.2012.  

kufahamu zaidi kuhusiana na kesi hiyo endelea kufuatilia Blog hii.

SABABU ZA KIFO CHA KANUMBA ZATAJWA

Baada ya utata kuhusiana na kifo cha nyota wa filamu Tanzania, Steven Charles Kanumba ambaye amezikwa jana katika makaburi ya kinondoni jiji Dar es salaam, hatimaye jopo la madaktari waliokuwa wakifanya uchunguzi kuhusu kifo hicho wametoa ripoti.

Jopo hilo la madaktari wapatao watano kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili wamesema kifo cha Kanumba kimetokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo ambalo kitaalamu linafahamika kama Brain Concussion.

Taarifa zaidi zinasema kuwa tatizo hilolinaweza kumsababishia mtu kupoteza maisha mara moja au baada ya siku kadhaa ambapo taarifa zimeendelea kusema kuwa tatizo hilo liligundulika baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa muda wa masaa mawili.

Aidha taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji ujulikanao kama Cardio-Respitory failure.
Hata hivyo baada ya uchunguzi imebainika kuwa kucha za marehemu zimebadilika na kuwa za Bluu wakati mapafu yake yalikutwa yakiwa yamevilia damu na kubadilika na kuwa kama maini.

Aidha taarifa hiyo imeendelea kueleza kuwa mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo anaweza kutokwa na mapovu mdomoni na kukoroma kabla ya kukata roho na kuthibitisha kuwa hicho ndicho kilichotokea kwa marehemu Kanumba.

Hata hivyo mmoja wa madaktari waliofanya uchunguzi huo amesema ubongo wa marehemu Kanumba ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji, wakati huo huo sehemu ya maini pamoja na majimaji ya machoni vimepelekwa kwa Mkemia mkuu wa serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu chochote kwenye mwili wa marehemu.

Tuesday, April 10, 2012

MAELFU YAFURIKA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA

Maelfu ya watu waliohudhuria katika shughuli ya kuaga mwili wa Steven Kanumba(Hapo ni wakati mwili wa mwrehemu ukiondoka Leaders na kuelekea makaburi ya kinondoni alipozikwa)

Makamu wa Rais Dk Bilal akiongoza maelfu waliojitokeza kuuaga mwili wa Steven kanumba

Mke wa Rais mama Salma Kikwete akiuaga mwili wa marehemu

Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe nae akiuaga mwili wa marehemu

Mbunge wa Mbeya mjini Mh. Joseph Mbilinyi(Sugu) naye akitoa heshima zake za mwisho kwa marehemu Steven Kanumba

Mmoja kati ya waigizaji wa siku nyingi na mtu wa karibu wa kanumba Dino, akielezea machache kuhusu mazishi ya kanumba na kwa upande wake ameelezea kama ni tukio la kihistoria, wakati akifanya mahojiano na EATV.
Askari wa jeshi la Polisi wakihakikisha hali inakuwa salama
                                                
Watu walithubutu kupanda juu ya mti ili mradi waushuhudie mwili wa marehemu kanumba kwa mara ya mwisho






Nilikuwepo pia kwa ajili ya kuripoti yaliyokuwa yakiendelea kwenye mazishi hayo.

Ndugu zetu wa chama cha msalaba mwekundu(Red Cross) walifanya kazi kubwa sana, maana watu wengi sana walikuwa wakidondoka.. Kwa kweli watu wengi sana alijitokeza kumuaga na kumzika marehemu Steven Kanumba na kila mmoja alionyesha kuguswa kwake kwa msiba huu ila mwisho wa siku tunaamini kuwa mipango ya mungu haina makosa kilichobaki tumuombee tu alale mahali pema peponi.. Amina.