Friday, November 2, 2012

NHIF YATOA ELIMU KWA WANAVYUO NACHINGWEA

Veronika Luanda akipewa maelekezo na mwakilishi wa NHIF Lindi Fortunata Kullaya wakati wa utekelezaji wa mpango wa elimu kwa wanachama wa NHIF,uliofanyika kwenye chuo cha uuguzi Nachingwea (NTC).
Mwakilishi wa NHIF na CHF Lindi Fortunata Kullaya akitoa elimu na uhamasishaji kwa wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea kufahamu umuhimu wa kujiunga na Mfuko huo.
Mratibu wa NHIF/CHF kwa chuo cha ualimu Nachingwea Abinery Mkanya, akiwasilisha majina ya wanachama waliojiunga papo hapo kwenye meza ya uratibu wakati wa zoezi la uhamasishaji.
Mratibu wa CHF Wilaya ya Nachingwea Masiah Nyoni, akifafanua maswali yaliyoulizwa kutoka kwa washiriki wa mafunzo ya elimu ya NHIF na Mifuko ya Afya ya Jamii (CHF) ambao ni wanachuo wa chuo cha ualimu Nachingwea (NTTC).
Fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni yanayohusu changamoto na maboresho katika NHIF na CHF yalitolewa,pichani ni Ally Ngilima mwanachuo wa mwaka wa kwanza chuo cha ualimu Nachingwea akitoa maoni.

No comments:

Post a Comment