Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar
Viongozi
wa Jumuiya mbili za Kiislam Kisiwani Zanzibar wanaotuhumiwa kwa makosa
tofauti ya kutoa lugha za uchochezi na kusababisha ghasia na vitendo vya
uvunjifu wa amani uliopelekea uharibifu wa miundombinu ya barabara
ambao leo walifikishwa Mahakama Kuu ya Vuga mjini Zanzibar, wamerudishwa
tena Rumande.
Kesi
hiyo ambayo inawakabili Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
Sheikhe Faridi Hadi Ahmedi na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho Sheikhe
Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid
Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na Ghalib Ahmada Omar iliitwa mahakama kuu kwa kutajwa baada ya kuahirishwa mwezi uliopita.
Hata
hivyo, kabla ya kutajwa tena kwa kesi hiyo, huku kukiwa na ulinzi mkali
wa Makachero wa Polisi na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, ndani ya
Mahakama hiyo kulizuka mabishano makali ya kisheria huku kila upande
ukionyesha ujuzi wao wa kisheria.
Kwa
upande wa Mawakili wa Watuhumiwa Bw. Salum Toufik na Bw. Abdallah Juma
Kaka, wakiwasilisha hoja mbalimbali za uvunjifu wa haki za watuhumiwa
ikiwemo ya kunyolewa ndevu wakiwa Rumande katika Chuo cha Mafunzo jambo
ambalo ni kinyume na uhuru wa kuabudu kwani wamesema ndevu kwa mashehe
ni sehemu ya ibada.
Baada ya
kuwasilisha hoja hizo, Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Bw.
Ramadhani Nassibu, akinukuu vifungu vya sheria vilivyopo kwenye Katiba
ya Zanzibar na kusema kuwa kama kuna haki zinazovunjwa na chombo
chochote ama mtumishi wa Serikali kuna mahala pengine pa kupeleka
malalamiko hayo.
Baada ya
mabishano hayo, Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar Mh. George Kazi,
aliamuru watuhumiwa wote warudishwe tena rumande hadi Novemba 20, mwaka
huu itakapokuja tena katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kwa kutajwa.
|
No comments:
Post a Comment