Wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM kutoka mkoani Mtwara |
Mh. Wassira akiwa na baadhi ya wajumbe wa mkutano huo
MATOKEO ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC katika kura
zilizopigwa juzi mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa Chama cha Mapinduzi
(CCM) yamevuja.
Huku
Mwenyekiti wa chama hicho kinachoiongoza Serikali, Rais Jakaya Kikwete
akitangaza jana kuwa matokeo hayo yatatangazwa leo pamoja na matokeo ya nafasi
za Makamu Mwenyekiti lakini tayari hadi jana mchana zaidi ya asiliamia 90 ya
wajumbe walisha jua matokeo hayo na kuanza kupongezana huku yale ya wagombea wa
bara yakiwekwa na idadi ya kura zao.
Ingawa
baadhi ya wajumbe wameoneshwa kushangazwa na idadi ya kura alizopata Katibu
Mkuu wa Chama hicho Wilson Mukama kwa kushika nafasi ya 9 huku Steven Wasira akiwaongoza.
Wanaodaiwa kushinda nafasi 10 Zanzibar:
Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif
Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri
wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.
Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto. Wanaodaiwa kushinda Bara Majina ya wajumbe wa Nec walioshinda bara na kura walizopata katika mabano ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira aliyeongoza kundi hilo kwa kupata kura 2,135, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba (2,093), Mwekahazina wa CCM, Mwigulu Nchemba (1,967), na Katibu wa UVCCM, Martine Shigela (1,824). Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi (1,805), Waziri wa Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa, Bernard Membe (1,455), Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo (1,414), Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Jackson Msome (1,207), Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (1,174) pamoja na Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Fenela Mukangara (984). SOURCE:http://mrokim.blogspot.com |
No comments:
Post a Comment