Tuesday, February 7, 2012

WATANZANIA WAMETAKIWA KUTUMIA TAASISI ZA SERIKALI


Leo kupitia kipindi cha Supermix cha East Africa Radio walialikwa wawakilishi kutoka kamati ya Amani, uzalendo mshikamano na maendeleo lengo kubwa likiwa ni kuhamasisha watanzania kuhusu matumizi ya Taasisi za serikali kama vile shirika la ndege la ATCL badala ya kutumia mashirika binafsi zaidi ili kuyafanya mashirika hayo yaendelee.

Risasi Mwaulanga(Katibu wa kamati)
Fikirini Saningo(Mjumbe)
Hillary Daudi a.k.a Zembwela mtangazaji wa kipindi cha Supermix


Kama nilivyoeleza hapo juu kuna hiyo kamati ambayo yenyewe kazi yake kubwa ni kuhamasisha utumiaji wa Taasisi mbalimbali za serikali ili kuzifanya Taasisi hizo zikue, maana sasa hivi tunaona mashirika au Taasisi zetu zinazorota, jambo ambalo wao kama wanakamati wamelifanyia uchunguzi na kubaini kuwa watanzania hatuna uzalendo wa kutumia hizo Taasisi zetu ila tunatumia zaidi Taasisi binafsi.

Wakatolea mfano mashirika ya ndege, mara nyingi watu hatutumii Shirika letu la ATCL na badala yake tunatumia zaidi yale ya binafsi na hata hao viongozi wa serikali ambao walitakiwa wawe mstari wa mbele kutuhamasisha wananchi ndio wanaongoza kwa kutumia hizo Taasisi binafsi, hivyo nami kupitita Blog hii natoa Hamasa kwenu watanzania wenzangu sasa tubadilike na tuanze kutumia Mashirika/Taasisi zetu za serikali.

No comments:

Post a Comment