Monday, February 6, 2012

JUMAMOSI ILIKUWA HIVI

Tulianzia  Kilwa Road Pub pande za JKT, pale kila Jumamosi kunakuwa na Police  Jazz Band  wakitumbuiza huyu ni mmoja kati ya waimbaji anaitwa "Afande Hamza", huwa anafurahisha sana kwa kweli kuanzia mavazi yake mpaka vituko vyake anapokuwa kwenye Steji
Huyu nae pia ni muimbaji ila sikupata jina lake si unajua watu walikuwa Busy huwezi kupata jina la kila mtu.
Afande Salum yeye si mpiga Drums tu pia ni mcheza Show machachari sana bahati mbaya sikupata picha yake wakati anacheza ila wakatri mwingine nitaziweka.
Mdada anaitwa Mariam a.k.a Maftah halisi ya kitanzania, ni bonge la mnenguaji wa Police  Jazz Band, kama ulifikiri maafande hawawezi kuchezesha nyonga basi utayaona mambo yao kupitia Afrobeat Jumamosi hii.
Mdada hadi mambo ya msamba anayaweza, kama unavyomuona akiwajibika kwa nyuma  pale ni Afande mwenzake "Khadija" kama akimshangaa hiviii.
Baada ya hapo safari ikaelekea pande za Temeke "Mpo Afrika" Pub hapo kuna mchakato wa kusaka vipaji kwa vijana wa Temeke inaitwa Temeke Star Search (TSS) mfumo wake ni kama ule wa BSS tofauti yake ni kwamba hawa ni bado wanaanza tu.
Jamaa anaitwa Toni Blair ndo muandaaji wa hiyo Temeke Star  Search  akielezea kuhusu mpango mzima wa hiyo  hilo  Shindano, usikose Afrobeat wiki hii ili kufahamu zaidi kuhusu shindano hilo.
Baadhi ya Majaji kutoka kulia ni Jumanne Idd mshindi wa BSS ya kwanza sikumbuki ilikuwa mwaka gani,  anaefuata ni Sister P na mmoja kati ya wanamuziki wa kundi la Mabaga Fresh.
Baada ya kufahamu kuhusu TSS kazi ikaanza sasa hapo nikiwa  najiandaa kufanya Links
Kwa kawaida huwa tunafanya Show zaidi ya moja kila wiki, incase anything happens show inaenda hewani kama kawaida 
Kimanyo kazini katika kuikamilisha Afrobeat... Haya mambo yote yatakuwa ndani ya Afrobeat wiki hii so stay tuned.

No comments:

Post a Comment