Thursday, February 9, 2012

SERIKALI YAVALIA NJUGA MGOMO WA MADAKTARI, WASIMAMISHA KAZI KATIBU MKUU NA MGANGA MKUU WA SERIKALI

Katibu mkuu wa Wizara ya Afya- Blandina Nyoni
Waziri mkuu Mizengo Pinda akiwasikiliza kwa makini madaktari leo jijini Dar es salaam, Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Hawa Ghasia na kulia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya Muhimbili Bi. Marina Njelekela.
 Serikali imemuandikia Barua ya kumsimamisha kazi Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bi.BLANDINA NYONI na Mganga Mkuu wa Serikali Dokta DEO MTASIWA ili kupisha uchunguzi dhidi ya malalamiko ya Madaktari.

Hata hivyo suala la Waziri wa Afya na Naibu Wake limeachwa kwa Rais JAKAYA KIKWETE kwa kuwa ndiye mwenye dhamana na Viongozi hao.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri Mkuu Mheshimiwa MIZENGO PINDA wakati akizungumza na Makundi kadhaa ya Madaktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya jitihada za kumaliza mgomo wa Madaktari.

Mheshimiwa PINDA amesema vyombo vya dola kwa sasa vinafanya kazi ya uchunguzi ili kubaini ukweli wa malalamiko hayo wakati watumishi hao wakiwa nje ya ofisi na kwamba atateuliwa Kaimu Mganga Mkuu na Kaimu Katibu Mkuu kuanzia sasa ili kushika nafasi hizo.






Aidha, mheshimiwa Pinda amesema serikali imekubali kuongeza kiwango cha posho ya kuitwa kazini kw madaktari hao sambamba na kuunda tume itakayoishauri kuhusiana na madai nane ya madaktari hao ikiwemo nyongeza ya mshahara ya shilingi milioni tatu na laki tano kama kima cha chini.

 Wakati huo huo, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepokea taarifa ya Kamati yake ya Huduma za Jamii ambayo ina mapendekezo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua ili kumaliza mgogoro unaoendelea kati ya Madaktari na Serikali.

Kufahamu zaidi kuhusu sakata hilo usikose kuangalia KURASA ya Eatv leo.

No comments:

Post a Comment