Thursday, February 2, 2012

KIKAO CHA HARUSI FACE TO FACE PUB

Kila Jumapili jioni huwa tunakutana pale Face to Face Pub maeneo ya makumbusho kwa ajili ya kikao cha harusi ya mmoja kati ya Mastaa wa bongo, hahaha najua ungependa kufahamu ni nani huyo anataka kuvuta jiko, endelea kufuatilia blog hii utamfahamu soon... pichani ni Mwenyekiti wa kikao hicho  Mussa Kondo "kushoto" na Mwekahazina Nicholas Sabai "kulia"
Kabla ya kikao kuanza maana kama unavyojua waswahili hatuwezi kabisa kwenda na muda hivyo tuliowahi ikabidi tuwasubiri wenzetu ndo kikao kianze
Tukasubiri wee ikabidi tuanze tu aliyechelewa atamuuliza jirani yake nini kimepita
Kikao kikiendelea, lakini kaka Kabyemela hapo Busy na Simu mambo ya BBM haya jamani!!!!




Sijui nini kilifurahisha hapo??? itakuwa Kabyemela tu huyo ndo alituchekesha maana ana vituko huyu kaka jamani...
Mauzo huwa haya kosi kwenye kitu chochote, hapo tukiuza sura na Happy mmoja kati ya watu wanaofanya watu wa Eatv tupate mishahara huyu maana anakukuruka kutafuta wadhamini
Marygoreth anapiga mkwara hapo asifotolewe eti watu wataiga Hair style yake, hahahhahha
Haya mapouzi, Jozee a.k.a Kabyemela
Mwenyekiti kulia na Katibu wake Prudence Gerald, mmependezaje?? kama ndo nyie vilee??... Kikao kitaendelea tena Jumapili ijayo na tunategemea mahudhurio yatakuwa mazuri zaidi na nyie wachelewaji mjitahidi kuwahi wiki hii.



No comments:

Post a Comment