Monday, February 6, 2012

MECHI YA HISANI KUCHANGIA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KATI YA BONGO MOVIES NA BONGO DANSI

Jana kulikuwa na mechi ya hisani kwa ajili ya kuchangia waathirika wa mafuriko kati ya Bongo movie na wanamuziki wa dansi nchini, matokeo ni Bongo movie walishinda bao 4 kwa 3 na kwa kweli watanzania tulionyesha uzalendo mkubwa sana maana ilikuwa nyomiiiiiii yaani watu kibao.. pichani hapo juu ni Benchi la Bongo movie.

Kikosi cha Wanamuziki wa Dansi
Mamaa Asha Baraka akiingia uwanjani, kiukweli huyu mama huwa anajitoa sana katika shughuli mbalimbali na jana alikuwa hashikiki yaani yeye ndo alikuwa mama pale uwanjani.
Kikosi cha Bongo movie unaambiwa waliingiza mamluki haoooo, wenyewe wakadai eti wote waliocheza ni wasanii na wana filamu zao ila bado hazijaingia sokoni, hayo yalikuwa ni maneno ya Ray hahahahhaa... utaona mwenyewe kupitia Afrobeat Jumamosi hiii.
Benchi la Wanamuziki wa Dansi hilo kama unavyomuona Iron Lady Asha Baraka sijui anaelekeza nini hapo.
Yaani ukikaa na hawa watu unaweza kuzimia kwa kucheka, kushoto hapo na Mkwere wa Mizwngwe ya ITV na Masanja Mkandamizaji
Chekibudi akiingia uwanjani baada ya Dr. Cheni kutoka, alicheza nafasi ya Goal Keeper ila cha kusikitisha huyu jamaa alimuumiza mguu mchezaji wa upande wa Dansi na inasemekana amevunjika mguu utamuona kwenye picha zinazofuata.
Hapo Bongo movie kabla ya mechi kuanza wakiingia uwanjani kabla ya mechi kuanza
Hawa ni moja kati ya waliotuburudisha siku ya jana, tulicheka weeee tukaongeza siku zetu za kuishi kwa raha zetuu.
Huyu ndo mchezaji ambae inasemekana kuwa amevunjika mguu kutoka timu ya Bongo dansi
Hawa nao ni moja kati ya wachekeshaji wakali Bongo, kushoto ni Dr. Rushwa wa Ze comedy ya Eatv na dada hapo kutoka Mizengwe ya Eatv.

No comments:

Post a Comment