Monday, February 27, 2012

JUMAMOSI ILIKUWA SCHENGEN ACADEMY

Jumamosi kama kawa kama dawa tulitinga ndni ya Hunters Club Kinondoni ambapo kama kawaida Schengen Academy wanakuwa pale kwa ajili ya kutoa burudani kwa wapenzi wa maeneo hayo
Mjomba Ngally kazini kuchukua kila tukio linaloendelea
Vijana kazini
Huyu ni muimbaji mpya kutoka Congo anaitwa Petii maana yake ni mdogo, jamaa ni mkali wa kuimba na kucheza yaani balaaaa
Huyu dada wakati wote yeye anafurahi tuuu mwanzo mwisho
Interview na Kiongozi wa Schengen Academy, Liva Hassan Sultan, kikubwa hasa nilitaka kujua kuhusu uchapakazi wake maana tangu tumefika yeye alikuwa anaimba mpaka mwiisho tofauti na viongozi au Mastaa wengine ambao hupanda Stejini mwishoni wakati show inakaribia kumalizika.. kufahamu nini ameongea endelea kufuatilia Afrobeat
Rapa wa Schengen, jamaa ni mkali sana ila bado tu hajapata umaarufu kama akina Totoo ze bingwa, Kanal Top na wengineo
Mpiga Gitar mwenyewe nasema alikuwa akifanya kazi na bendi kubwa za kongo na hapa bongo hakuna anayeweza kumfikia kabisaaaa, anaitwa Le Mapenzi cjui maana yake nini?? nilimuuliza akaniambia ataniambia siku nyingine na hiyo siku lazima nifanye nae Interview ndo atasema
Massano na Ngally kutoka Eatv wakiwajibika

Unamkumbuka huyuuu? Anaitwa Amina alikuwa mmoja kati ya washiriki wa manywele kimwana wa Twanga pepeta 2011 na kwa sasa yupo Schengen Academy anapiga kazi

No comments:

Post a Comment