Monday, February 20, 2012

BONGEA LA MECHI KATI YA FNB HEAD OFFICE NA FNB BRANCH PANDE ZA TAMBAZA HIGH SCHOOL


Jumamosi kulikuwa na bonge la mechi kati ya FNB Head Office na FNB Branch katika uwanja wa Tambaza High school yaani tulihave fun kiukweli, kwanza baada ya kufika kabla ya mechi tulijifotia wee kama unavyoona hapo juu, Kushoto ni Ezekiel na Andy kutoka Branch na Moggy mmoja kati ya marafiki ambao walijumuika na marafiki kushow luv

Andy, kijah na Eze
Timu zikijiandaa na mchezo hiyo ni timu ya Branch, walitinga uzi wa kijani, Muga alichelewa kufika na aliwahi kuchoka utaona huko chini mambo yake
Timu pinzani Head Office, mie nilikuwa shabiki wa Timu ya Branch kwa sababu maalum
Haya sasa kazi imeanza naona timu yetu ikijipanga kwa maangamizi
Hapo goli likiingia sijui lilikuwa la ngapi hili, but ma boy Andy ndo alifungua dimba kwa kuipatia Timu yake bao la kwanza
Andy akijaribu kumtoka mpinzani, ila walikimbizwa hawa jamaa wa Head Office hadi huruma aiseh
Mashabiki wakifuatilia mchezo, wengi wao walikuwa ni mashabiki wa Branch
Mimi, Mona,Lilyan, Angel na Oliver
Sasa huyu ndo Muga hapo yuko hoiiiii, unaambiwa jamaa hachoki wa haumii, hahahahhahhhaha
Choka mbayaaaa dakika 90 siyo mchezo jamani, yaani huyu Refa(mwenye T-Shirt nyekundu) alinifurahisha sana jamani yeye alikuwa hakimbii wala nini kasimama tu katikati kama unavyomuona
Baada ya game kumalizika ambapo branch waliondoka kwa ushindi wa Bao 7 kwa 2, chezea Brach yaani wanawafunga hadi maboss wao??!!!!
Kila siku ni Furahiday siyo lazima iwe ijumaa
Baada ya Dakika 90 watu choka mbayaaaaaaa
Poleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!
Picha ya ushindiiiiiii
Tulikula na tulikunywa pia kama uonavyo, hayo majiko yalikuwa kama matatu hivi, ila mpigapicha wetu sijui vipi kapiga moja, moja
With frands Angel, Oliver na Lily, yaani sisi ilikuwa ni mwendo wa picha tuuuuuuuuu kwa raha zetuuu, nilifurahi sana kukutana na nyie girls maana tulipiga story utafikiri tulifahamiana kabla ya hapo
Neno la shukrani kwa wote waliokuja, hapo tukapewa somo kila mwenye kinywaji tafadhali kopo/chupa yake asitupe ovyo aiweke kwenye vifaa maalum vilivyowekwa maana si unajua wakati mwingine kwenye watu wengi kuna mambo ukizingatia kila mmoja ana ustaarabu wake wa huko alipotokea
Jamaa kama akisema Brach oyeeeeeee

Neno la shukrani kutoka kwa HR Manager Mr. Materu na akasema inabidi Mechi irudiwe haiwezekani madogo mtufunge wakubwa wenu
Umegundua chochote kwenye hii picha?
Nilikuambia sie ni picha tu jamani maana hata mpiga picha mwenyewe alikuwa akitamani kutufotoa kila wakati kila tukihama tunae, tukibadilisha pozi huyoo
Mechi ijayo inabidi tuwafunge zaidi ya leo ikwezekana tuwapige kumi au unasemaje Andy(hahahhahhahha)
Iman wenyewe wanatamka Aiman

1 comment:

  1. Jamani mnaoniambia mnashindwa kucomment inakuwajeee?? mbona ni rahisi tu km hiviii?

    ReplyDelete