Monday, February 6, 2012

ASHA BARAKA KUSAKA VIPAJI VYA WAPIGA ALA ZA MUZIKI

MKURUGENZI wa Kampuni ya The African Stars Entertainment ASET, Asha Baraka ametangaza kutoka kivingine kwa kuanzisha Taasisi ya kuvumbua vipaji itakayokwenda kwa jina la Twanga Academia.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika mkutano uliofanyika Katika ukumbi wa Mango Garden Dar es Salaam  jana, Asha Baraka amesema kwamba Twanga Academia wamenunua vifaa vyenye thamani ya sh. Mil 100 kwa kuanzia.
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa katika taasisi hiyo wamepanga kufanya usaili uliopangwa kufanyika Jumapili ijayo February 12 katika viwanja vya Leaders Club, ambapo usaili huo utaanza saa sita mchana.


Baraka aliongeza kuwa usaili huo utasimamiwa na magwiji wa muziki wa dansi nchini ambao pia ni wanamuziki kama Hamza Kalala ‘ Mzee wa Madongo’ na wengineo kadhaa ambapo watatoa fursa kwa chipukizi wanye uwezo wa kutumia ala za muziki.

No comments:

Post a Comment