Friday, February 3, 2012

ISHA MASHAUZI AWEKA WAZI KUHUSU UHUSIANO WAKE NA THABIT ABDUL

Mwanadada anayekimbiza katika muziki wa Taarab nchini ambae pia ni Mkurugenzi wa kundi la Mashauzi Classic lenye makazi yake jijini Dar Es Salaam, Isha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi amemefunguka kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki na kiongozi mwenzake wa kundi hilo la Mashauzi Classic "Thabit Abdul"
Akizungumza na kipindi cha Afrobeat ya Eatv hivi karibuni kati ya mengi aliyozungumza ni pamoja na uhusiano wake na mwanamuziki huyo.

Isha amesema pamoja na uvumi ulioenea huko mtaani kuwa yeye(Isha) ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki huyo ambae anasifika kwa utaalam wake wa kukung'uta kinanda lakini ukweli unabaki kuwa uhusiano wao upo kikazi zaidi na si tofauti na hilo.

Amesema amesikia watu wengi wakiwa na mashaka juu ya uhusiano wao na hata wanapokuwa kwenye ziara za kimuziki katika mikoa mbali mbali hapa Nchini watu wengi wamekuwa wakihoji kuhusu hilo lakini anaamini kuwa hiyo inatokana na ukaribu wao na utani walio nao ambao wakati mwingine huwa wanaitana majina yenye utata kama vile baby, Darling na mengineyo ya aina hiyo, hivyo amewataka mashabiki kutomfikiria vibaya na waamini kuwa huo ni utani tu unaofanya hata kazi zao kuwa bora zaidi.

Endelea kuangalia Afrobeat kila Jumamosi saa moja jioni ili uweze kumsikia mwenyewe akizungumza mengi zaidi ya hayo, ni kupitia Ting'a namba moja kwa vijana! Eatv

No comments:

Post a Comment