Monday, February 13, 2012

TWANGA ACADEMY WACHUKUA FOMU

Wiki iliyopita nilikueleza kuhusu mpango wa ASSET ikiongozwa na mkurugenzi Asha Baraka kwa kushirikiana na Urban Pulse kuhusu kusaka vipaji vya wapiga vyombo, waimbaji na wanenguaji pia, Jumapili hii(jana) zoezi la kuchukua Fomu limeanza na Afrobeat tulizungumza na baadhi ya wahusika ili kufahamu Lengo hasa la mchakato huu ni nini?
Manager Urban Pulse Creative (Tanzania) Nocha Sebe akielezea kuhusu Lengo la wao kuanzisha mchakato huu ambapo kubwa zaidi ni kusaka vipaji hasa kwa upande wa wapiga vyombo baada ya kugundua kuwa Tanzania kuna vipaji vingi sana lakini vinakosa nafasi ya kutokea na kuonyesha vipaji vyao, pia wamebaini kuwa baada ya miaka mitano ijayo inawezekana kusiwe na wapiga vyombo kabisa kutokana na waliopo kuwa watu wazima sana.
Gwiji la muziki Tanzania Hamza Kalala ambae pioa ni Jaji na mkufunzi wa mashindano hayo yeye anasema amefurahishwa sana na mashindano hayo na atajitoa kwa kadri ya uwezo wake ili kuibua vipaji vingi vilivyopo mtaani, kama alivyoibua vipaji vya watoto wake Kalal Junior na Totoo Kalala pia mastaa wengine hapa Bongo kama vile Ally Choki naMwinjuma muumini
Watu busy na kazi yao mwenye kofia ni William Massano Soundman, Cameraman Rajab Kimanyo na mimi (Kijah) wakati wa Mahojiano na Hamza Kalal Komandoo a.k.a Mzee wa Madongo
Mmoja kati ya waliochukua fomu jumapili hii yeye ni muimbaji na alituimbia pia, anaweza sana kiukweli ila siwezi kusema kuwa atashinda maana wanaoweza nao wanazidiana, hapo akituonyesha fomu yake.. Ili kuona ukali wake angalia Afrobeat Jumamosi hii

No comments:

Post a Comment