Hata hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji, huku taarifa zaidi ikifafanua kwamba hakuna mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechomwa moto. Nyumba ya mwandishi wa Habari wa TBC kassim Mikongoro inasemekana Imechomwa moto mchana huu.Hali ni tete Askari wawili na raia mmoja wanasadikika kuuawa.
Wakati huo huo Spika wa Bunge la Jmhuri wa Muungano wa Tanzani Anne Makinda ameahirisha Kikao cha Bunge mpaka kesho ambapo ameiagiza serikali kuja taarifa kamili kuhusiana na vurugu zinazoendelea huko Mtwara.
No comments:
Post a Comment