Monday, October 17, 2011

USIYOYAJUA KUHUSU AISHA MADINDA

Aisha madinda akiimba wimbo  wa Mbiliabel  (Eswi yo wapi)
Aisha akiwa katika ajira yake tuliyoizoea ya Unenguaji


Siku chache zilizopita mnenguaji kiwango cha juu hapa Bongo anayefanyia kazi katika Bendi ya Extra Bongo, Aisha Madinda aliwaacha hoi mashabiki wake baada ya kuwaburudisha mashabiki hao kwa kuimba nyimbo mbalimbali ukiwemo wimbo wa Mwanamama Mbiliabel (Eswi yo Wapi)

Akizungumza na Blog hii Aisha alisema ameamua kufanya hivyo ili kuwapa burudani mashabiki wake na katika kuwaonyesha kuwa yeye ni mkali na ana vipaji vingi ukiacha unenguaji ambapo ameanza kuonyesha kipaji chake hicho cha kuimba na akishazoeleka katika Fani hiyo ataendelea kuwashangaza mashabiki wake kwa kuwaonyesha kipaji chake kingine.

Pamoja na kuzungumzia vipaji vyake hivyo ambavyo vingine hakupenda kuviweka wazi kwa sasa kwa madai ya kuwa ni mapema mno, Aisha aliweka wazi baadhi ya vitu anavyovipenda na ambavyo huwa anavifanya nje ya kazi yake ya Muziki ambapo alisema kuwa yeye ni mjasiriamali ambae hujishughulisha na biashara mbalimbali ambazo huzifanya kwa muda wake wa mapumziko.

Aidha Aisha ni mpenda michezo hususani Football ambapo kwa hapa bongo ni shabiki mkubwa wa Timu ya Simba na huko nje ya Nchi anaipenda sana Timu ya Mashetani wekundu(Manchester United "Man U")

Aisha ambae amezaliwa May 5, 1980 ingawa hajaolewa lakini ni mama wa watoto wawili wa kwanza ni wa kiume na wa pili ni wa kike, akiwa nyumbani anapendelea sana kufanya usafi wa nyumba yake pamoja na kupika na chakula ambacho hupendelea zaidi ni ndizi nyama.

Mwisho nilimuuliza swali la kizushi kuwa anapendelea mwanaume wa aina gani? Jibu lilikuwa hivi "awe mrefu asiwe mwembamba sana na asiwe mnene na pia awe anayejua mapenzi" upo hapooooooooo????

No comments:

Post a Comment