Monday, October 10, 2011

SUPERMIX YA EAST AFRICA RADIO YAONGEA NA RIDHWAN

Kweli mtoto wa nyoka ni nyoka jamaa kila wakatia anasmile, yaani like father like son hapo ilikuwa kabla hajaanza Interview

Hii ilikuwa kwa ajili ya Halla 5 ya E news, huyu jamaa alikuja nae but sikupata jina lake


Huyu jamaa anaitwa Dickson Tegemea mmoja kati ya Staff wa Eatv akichukua picha kwa ajili ya vipindi vyetu vya TV nyuma yake ni Michael Baruti Presenter wa Super Mix
Ijuumaa ya October 7 ilikuwa ni Birthday ya Rais wetu JK ndipo kipindi cha Supermix cha EARADIO kinachoendeshwa na Michael Baruti kwa kushirikiana na Hillary a.k.a Zembwela Beberu kikamkaribisha Ridhwan ili kuongea nae mawili matatu kuhusiana na yeye mwenyewe familia yao pamoja na JK mwenyewe na kiukweli alifunguka hasa, sanasana ilikuwa katika maisha yao ya kawaida tu.

Alielezea kuhusu uhusiana wake yeye kama Rais na familia yake uko kama zamani au mambo yamebadilika kutokana na wadhifa alionao, ambapo majibu yalikuwa rahisi tu kuwa hakuna kilichobadilika pamoja na majukumu kuwa mengi lakini anajitahidi kuwa karibu na familia japo haipo kama ilivyokuwa mwanzo.

Kwa upande wao kama watoto alieleza kuwa kutokana na malezi waliyolelewa na baba yao ya kujichanganya na kila mtu, wao wamekuwa ni watu wa watu na kwa sababu wanapenda kujichanganya na hawajichukulii tofauti na watu wengine kutokana na wadhifa wa baba yao.

Aliendelea kuweka wazi kuwa wakati wakiwa wadogo baba yao alikuwa na tabia ya kuwapeleka kijijini kwao ili waweze kuzoea maisha ya kule na ndivyo ilivyo sasa mara kwa mara wamekuwa wakitembelea kijijini kwao na mpaka watoto wao wanawalea kwa malezi hayo ya kujichanganya na kupendelea kuwapeleka kijijini kwao.

Alizungumza vitu vingi sana ikiwa na vitu ambavyo JK anapendelea, kwa upande wa muziki alisema anapendelea sana kusikiliza nyimbo za zamani na hata za sasa baadhi lakini anazozipenda sana ni zile za MV mapenzi na Homa imenizidia kwa zile za enzi hizo. Kwa upande wa chakula alisema anapenda sana vyakula vya asili kama ugali wa muhogo na mboga za majani.. Kwa upande wa mchezo anapendelea sana Football na Basketball ambapo kipindi cha nyuma alikuwa akicheza pia mchezo huo na Timu azipendazo kwa hapa Bongo ni Yanga na huko majuu anaipenda sana Timu ya Newcastle United.

Akizungumzia kuhusu adhabu aliyokuwa akipenda kutoa kwa watoto wake amesema JK hakuwa mtu wa kutoa adhabu zaidi ya kuelekeza tu ila kwa upande wa mama yao(Salma Kikwete) alikuwa akitoa adhabu ndogo ndogo za kufanya kazi za nyumbani kama kuosha vyombo na nyinginezo ambazo anaamini ndizo zilizowafanya wawe na maadili mema mpaka sasa.

Alizungumza vitu vingi sana tu lakini vingi ni vile vinavyofahamika nikaona nidonoe vichache ambavyo havifahamiki ili niwapatie wadau.

No comments:

Post a Comment