Monday, October 10, 2011

AJALI NYINGINE MKOANI LINDI

Baadhi ya abiria waliokuwa wakisafiri kwa basi la Ng'itu lenye namba za usajili T 804 BAF wakiingia ndani ili kuokoa abiria wenzao waliokandamizwa na seat ndani ya basi hilo ambalo kwa uwezo wa mungu hakuna aliyepoteza maisha ila wapo baadhi walioumia

Baadhi ya abiria wakisaidiana kulinyanyua basi hilo ili kuokoa maisha ya baadhi ya abiria waliokandamizwa na basi chini ya basi hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Lindi bw. Ludovick mwananzila pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam bw. Said Mecky Sadick wakipata maelezo ya namna basi hilo lilivyopata ajali kutoka kwa mmoja wa abiria wa basi hilo.


Mkuu wa mkoa wa Lindi bw. Ludovick mwananzila akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa bw. Nurdini Babu ahakikishe kuwa majeruhi wanakimbizwa hospitali na abiria wengine wanapata usafiri wa haraka na kuamuru magari yaliyomo kwenye msafara wake yanasaidia kubeba majeruhi hao (Nyuma ni mkuu wa mkoa wa DSM bw. Sadick)


Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es salaam kwenda Mtwara kwa Basi
la Ng’itu lenye namba za Usajili T 804 BAF wamenusurika kifo baada ya
basi hilo kupinduka katika kijiji cha Sinza –Miteja wilayani Kilwa, mkoani Lindi  

Katika ajili hiyo zaidi ya abiria 35 waliumia vibaya na kukimbizwa
katika hospital zilizo jirani na eneo hilo

Ajali hiyo iliyotokea jana jioni ilishuhudiwa na Wakuu wa Mikoa ya Dar es salaam na
Lindi,Saidi Meck Sadiki na Ludovick Mwananzila walipokuwa katika
Makabidhiano ya Mkoa huo kufuatia Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufanya
mabadiliko ya vituo kati ya Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Lindi, Ally Nassor
Rufunga kubadilishana vituo na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Ludovick Mwananzila kupangiwa Lindi
 
Chanzo cha ajali hiyo kwa Mujibu wa Abiria walioongea na Mdau wa blog
hii wameeleza ni mwendo kasi uliochangiwa na kufukuzana kwa mabasi
yaliyoongozana kuelekea Tunduru,Masasi,Nachingwea na Newala
 
Taarifa hii imeletwa na mdau Abdulaziz video Rec aliyeshuhudia ajali
hiyo aliyefika dakika 5 baada ya ajali kutokea.

No comments:

Post a Comment