Tuesday, October 25, 2011

UNAMKUMBUKA MAREHEMU FRANCO???

Picha zote hapo juu zinamuonyesha Marehemu Franco katika matukio mbalimbali ya shughuli yake ya Muziki

Jina lake halisi lilikuwa ni Francois Luambo Makiadi lakini alikuwa maarufu kama Franco Luambo, alizaliwa July 6, 1938 katika kijiji cha Sona-Bata huko DRC  na kufariki October 12, 1989 akiwa na watoto 18.

Alianza kupenda muziki akiwa na umri mdogo sana na alipofika umri wa miaka 7 alitengeneza Gitaa lake ambalo alikuwa akilipiga sokoni ambapo mama yake alikuwa akifanya biashara ya mikate kwa lengo la kuwavutia wateja.

Muziki wake kwa mara ya kwanza ulirekodiwa na kuwekwa kwenye Tape na mpiga Gitaa Paul Ebengo Dewayon ambae baadae alimchukua na kuanza kumfundisha namna ya upigaji wa Gitaa kitaalamu na mara ya kwanza alianza kupiga show akiwa na Band ya Dewayo akiwa na umri wa miaka 12. Lakini pamoja na kupiga Gitaa na vyombo vingine, Franco alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kuimba kama unavyoona kwenye picha akiimba na wakati huo huo anapiga Gitaa

Mwaka 1953 alitoa wimbo wake alioupa jina la Bolingo na ngai na Beatrice(My love for Beatrice) na baadae mwaka 1956 alianzisha band iliyoitwa OK Jazz ambayo baadae ilibadilishwa na kuwa TP OK Jazz, Band ambayo ilikuwa kutoka wanamuziki 6 mpaka 50 miaka 30 baadae ambapo iliendelea kuwa juu na kutengeneza album zaidi ya 150 ambapo kila album iliweza kuuza zaidi ya Kopi 50,000.

Nimekuletea habari hii leo katika kukumbuka miaka 22 tangu kifo cha mwanamuziki huyu ambae amechangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa muziki wa Dansi barani Afrika.. 

R.I.P FRANCO

No comments:

Post a Comment