Wednesday, October 5, 2011

K-MONDO SOUND KUWATAMBULISHA DK. KUMPENEKA NA IMANI LISU JUMAMOSI HII NDANI YA ZHONG HUA GARDEN

Dk. Kumpeneka kazini

Imani Lissu akiwajibika

Ibonga katumbi a.k.a Jesus (kushoto) na Roger mulondanyi a.k.a muzungu

MASHABIKI wa K-mondo Sound Band Jumamosi hii watapata fursa ya kuwaona kwa mara ya kwanza waimbaji wapya waliojiunga na Bendi hiyo Imani Lisu akitokea BSS Second Chance na Dk.Kumpeneka aliyetamba na kibao Dokta wangu miaka kadhaa iliyopita wakati wa utambulisho wao katika ndani ya Zhong Hua Garden Jumamosi hii.

Pamoja na kwamba itakuwa ni siku ya utambulisho wa wanamuziki hao wapya lakini pia itakuwa ni mara ya kwanza kwa K-Mondo Sound kupiga Zhong Hua Garden. Burudani hiyo ya K-mondo Sound itasindikizwa na mwimbaji mkongwe Ibonga Katumbi 'Jesus' ambapo pia Jesus atatambulisha jina lake jipya. 

No comments:

Post a Comment